Tetesi: Polisi Kutopenda Maridhiano: Kuzuia Fujo ni Fursa ya Kipato

...Unapo watawanya wanatawanyika, kisha wezi, majambazi na vibaka ambao hawana itikadi au waweza kuwa na yeyote hata ccm wanachukua nafasi ili watimize makusudio yao...
Kama CHADEMA wanafahamu hili kwa nini wanalazimisha litokee?
 
Nilitegemea WanaCCM ndo waandamane maana ndo waliomchagua kwa Kura nyingi. CCM majimbo 190 UKAWA (UKUTA) Majimbo 36. Democrasia ya kweli Wengi wanaamua si wachache na ndio maana Uchaguzi ulifanyika ili chama kitakachoshinda kipewe Ridhaa. Mkiendelea na maandamano ya kipuuzi na kupinga maendeleo CCM itatawala milele. UKUTA ( Ukitaka kuvunjika uti wa mgongo andamana)
 
kazi na dawa, kama vipi acha pesa na simu home, ila ukiwa mikono mitupu utatukoma.
 
Kimsingi UKAWA kwa serikali hii ya Magufuli hawana jipya mbali na maandamano na Matamko yasiyotekelezeka . Yale waliyokuwa wanayataka JPM anayafanyia kazi
 
Katiba ipi inayoruhusu kufanya fujo na kuachwa? Katiba ipi inaruhusu mtu kuhamasisha uvunjifu wa amani na police wasitoe warning?

Taja vifungu vya katiba vinavyosema police wanatakiwa kukaa kwenye mikutano ya maridhiano.

Jeshi la police lipo kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano Tanzania. Na majukumu ya police yametajwa kwenye sheria za jeshi la police.

Police wanaruhusiwa kutumia nguvu au kuua yule anayekaidi maagazi halali ya serikali.

Wewe umeambiwa hakuna kuandamana kwa mujibu wa taarifa za kiulinzi. Na mahakam imeridhia hivyo. Sasa wewe unaitisha vikao na police vya nini sasa. Ukitii sheria utawaona police wazuri sana.

Hakuna maridhiano wala mazungumzo amri imetolewa full stop.

Na police wamejiandaa kisawa sawa.
 
Hiyo ni kweli Mkuu.
Siyo jambo la siri. Ndio maana maandamano yanapotokea polisi hufurahi sana kwani wanajua ni fursa kwao. Baadhi ya pesa zilizoporwa hupelekwa kwa wakubwa walio watuma. Hiyo inajulikana kuanzia Polisi Makao Makuu mpaka vituo vyote vya polisi nchini. Yakiwa maandamano ya wanafunzi, polisi hufikia hatua ya kuingia ndani kusaka laptop kwa kisingizio cha kutafuta waarifu. Kama unavyoona wale polisi waendesha pikipiki halimaarufu kama Tigo, kazi yao kubwa ni kuchukuwa rushwa kwa waarifu na kila group limepewa kiasi cha kurejesha jioni kwa wakubwa. Hiyo ndo Tanzania ya SIJARIBIWI.
 
kazi na dawa, kama vipi acha pesa na simu home, ila ukiwa mikono mitupu utatukoma.
Mkuu wewe najua uko Mwanza, hebu sema ukweli zile fujo za 2010 kuhusu kutangaza matokeo ya ubunge kisha zikapelekea jiji kuchafuka, mawe makubwa kuwekwa barabarani na majengo kuchomwa moto ikiwemo Ofisi ya Ccm Nera jee Polisi waliweza kudhibiti? Mpaka waliomba kauli za wanasiasa kutuliza. Kule Mbeya nako wamachinga waliligeuza jiji lao kuwa uwanja wa mapambano hadi akaitwa Sugu toka Dodoma kuja kutuliza na wakatulia na kushika Fabio kufagia jiji.
Polisi wanajua kuwa kikiwaka hasa hawawezi kudhibiti ila wanapenda kiwake ili nao wapate FURSA maana maisha magumu.
Hata yote yanaweza kutoweka kama mfano Leo IGP akatoa tamko kuwa mikutano ruksa ila tuu taratibu zifuatwe kama zamani.
 
Sorry unazungumzia Jeshi la Polisi au genge la CCM?? Waulize wako wapi askari ambao waliahidiwa vyeo mwaka jana ili wahakikishe CCM wanarudi madarakani?? Hawapo, hakuna chochote cha mana kilichofanyika zaidi ya kuongezea posho hahahaa yaani uuze utu wako kwa ajili ya Posho??
 
Mkuu sasa nimekuelewa na wewe ndio umeenda kwenye mada hasa.
Kwa hiyo kumbe kila kitengo kina kula yake aka FURSA.
Yaani wa barabarani ndio hivyo tena inajulikana, Upelelezi ni kubambika kesi, mapokezi ni dhamana ya kutoka kituoni na FFU tuliokuwa hatujui wanakulaje ni hayo maandamano, fujo za mijini, vyuoni kwa wanafunzi nk nk. Ila hawa style yao ni ya kiuporaji zaidi.
 
Likewise usikaririshwe kwamba polisi wanaanzisha vurugu kwa lengo la kuwaibia raia mali zao, huko ni kufilisika kiakili
 
Likewise usikaririshwe kwamba polisi wanaanzisha vurugu kwa lengo la kuwaibia raia mali zao, huko ni kufilisika kiakili
Tusaidie wewe, kwa akili yako Polisi wanaanzisha hizo fujo kwa sababu ya nini?
 
Tusaidie wewe, kwa akili yako Polisi wanaanzisha hizo fujo kwa sababu ya nini?
Tusaidie wewe, kwa akili yako na ushahidi ambao tunaweza kuutumia kisheria, ni wapi polisi walianzisha fujo, then kuanzia hapo tunaweza kuchunguza kujua chanzo cha fujo hizo. otherwise, haya yote ni majungu na ushibiki ambao legally speaking dont hold water and you better tell to the marine!!!!!
 
Ulishawahi kuona wapi jeshini kunamaridhiano? Watu wengine wajinga sana hili ni jeshi la polisi siyo polisi jamii maridhiano yanatoka wapi
Kwahiyo ni kweli kwamba mnakwapua simu za wananchi ?
 
tutakua na mabango tuu mifukoni empty labda tuvuliwe nguo ila bado tutavaa magagulo
 


Siku zote waazisha fujo ni polisifisiem
 
Na kwenye opersheni haramu hizo hulipwa posho kubwa mno. Si unajua hata biashara haramu kama za madawa ya kulevya zinakuwaga na faida kubwa.
Ila chuki kwao ndio inaongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…