PRESS RELEASE
Hivi karibuni Taifa limeshuhudia kauli mbalimbali za baadhi ya wananchi wa kutoka kisiwa cha Pemba hususan wafuasi wa chama cha CUF za kutaka kujitenga kutoka ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iii waunde Serikali yao ya Pemba. Nia ya wananchi hao ya kutaka kujitenga, ilitolewa vile vile mbele ya Balozi wa Marekani hapa nchni wakati alipokitembelea kisiwa hicho. Baadaye tulishuhudia wananchi 12 wafuasi wa chama cha CUF na wakazi wa Pemba wakipeleka waraka wao wa kuomba wajitenge na Zanzibar kwenye ofisi za Umoja wa mataifa zilizoko Dar es Salaam.
Ufuatiliaji uliofanywa na Jeshi la Polisi umeonyesha kuwa harakati hizi za baadhi ya wananchi wa Pemba na ambao ni wafuasi wa chama cha CUF kutaka kujitenga na kuunda Serikali yao ya Pemba zimechochewa zaidi na uamuzi wa halmashauri Kuu ya CCM ilipoketi huko Butiama na kuelekeza kwamba suala la kuundwa kwa Serikali ya Mseto Zanzibar lirejeshwe kwa wananchi iii watoe maoni yao.
Si nia ya Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa yanayoendelea hapa nchini. Na wala hayo siyo majukumu yake. Hata hivyo malumbano yoyote ya kisiasa yanatakiwa yawe ya kistaarabu, ya kuvumiliana ya kupingana bila kupigana, na yasiyo na mwelekeo wa kuchochea vurugu, au uvunjaji wa amani.
Kwa ujumla, pamoja na haki ya kikatiba na kisheria ya kuendesha harakati za siasa za vyama vingi, haki hizo pia zina wajibu wake kwamba viongozi wetu wa vyama vya siasa pamoja na wafuasi hao, wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wanatii na kuheshimu sheria za nchi.
Kitendo cha baadhi ya wafuasi wa CUF na wakazi wa Pemba cha kutaka kujitenga kutoka ndani ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ni cha uvunjwaji wa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jeshi la Poslisi, likiwa ndicho chombo kinachosimamia na kulinda sheria za nchi, hali wezi kukaa kimya na kuendelea kushuhudia baadhi ya wananchi wakikiuka Katiba ya nchi ambayo ndiyo mhimili na msingi ya Demokrasia na amani tuliyonayo hapa nchini.
Kwa mantiki hiyo, tunawasihi wanasiasa wote hapa nchini waendeshe siasa zao kwa misingi iliyowekwa na Katiba na sheria za nchi. Nje ya hapo ni ukiukwaji na uvunjaji wa sheria za nchi.
Kwa ajili hiyo, nia au matakwa yoyote, pamoja na harakati zozote zinazofanywa za kisiwa cha Pemba kutaka kujitenga kutoka ndani ya Serikali ya mapinduzi Zanzibar kina lengo la kutaka kuathiri na kuvuruga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo imeundwa na Katiba. Kitendo hicho ni cha uhaini.
Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi limeanza kuchukua hatua za kisheria za kuwakamata na kuwahoji watu wote wanaotajwa kujihusisha na njama hizo iii wachukuliwe hatua za kisheria.
Kwa mara nyingine, tunawasihi viongozi wote wa kisiasa, pamoja na wafuasi wao wajenge utamaduni wa kuheshimu na kuzingatia sheria za nchi, pamoja na kuzitumia katika madai yoyote pale wanapodhani hawakutendewa haki. Huo ndiyo utawala wa sheria.
Ahsanteni sana.
S.A. MWEMA
INSPEKTA JENERALI WA POLlSI