Mzee mwanakijiji!!
Wapemba wanatamani warudi ktk utawala wa kiarabu kuliko kuongozwa na serikali ya sasa.
Mutu mwene akili timamu unaweza tamani kurudi ktk hali ya ukoloni?
Ni hatari ngapi ziliwakuta vongozi wetu ktk harakati za kumwondoa mwarabu na usheenzi wao zenj?leo hii mkombolewa anatamani kurudi alikotolewa!!!!
Kutaka kujitenga kwa wapemba si akili zao tuu,ni nguvu toka nje inayotaka kurudisha utawala wake,na hasa waarabu wanafahamu kuna damu yao waliiicha zenj,wana mikakati mizito ya kurudi na kuikomboa,sasa sioni mantiki ya kukombolewa kwa hao wakoloni waliobakia zenj,kwa gharama za wazenj weusi!!!!
Kama lengo ni ukombozi,njia rahisi ni hao wapemba kuomba kuondolewa kwa waarabu wote walioko zenj kurud makwao,na hiri ri nia litatusaidia sana.hasa ukizingatia hatuna tunahopata kupitia hawa wakoloni,sana sana wanatuchefua tuuuuuu
Kumekucha
Watz tuamke,hasa wapemba,ukoloni ulitutesa sana tena sana,hatuna haja ya kushabikia mwarabu au mjerumani na mreno,tazameni yaliyo bora kwenu,kumbukeni damu za weusi zilimwaga kwa wingi,leo hii tunajivunia ardhi tulionayo.
Dini na waanzilishi wake,visituchanganye kichwa,utu wetu watu weusi ni almasi kuliko kutetea maslahi ya wakoloni.
Black power forever.
Unaonyesha huna ulijualo hii ndio tabu ya kukurupuka alimradi upo katika mradi wa kufurahisha wengi na kuwaudhi WaPemba pole sana.
Embu nitajie hatari moja tu unayoijua wewe ambao iliwakuta manamba waliokwenda kulima mashamba ya karafuu na minazi ?
Hivi kwa akili yako ni wapi kwenye waarabu wengi kati ya Zanzibar na Tanganyika hadi burundi rwanda na Zaire ?
Unadai kuondoka kwa Waarabu mimi sitawaita hivyo bali nitasema watu weupe ,itazame Zimbabwe na kuwafukuza wazungu na kuyachukua mashamba ni kitu gani kimefuata na leo Zimbabwe ambao fedha yao ilikuwa sawa na kiwango cha dola ,sema basi au kataa kama Wazimbabwe hawatamani kurudi kwa wazungu ,hivi unajua historia ya Mugabe nini alifanya hata akatwaa madaraka na hao manamba walioiondoa serikali iliyopokea Uhuru Zanzibar kuna tofauti na alichokifanya Mugabe.
Labda kwa vile wewe unaamini walioondolewa Zanzibar ni waarabu na waliopinduliwa ni waarabu ,siwezi kukulaumu kwani ni kutokana na uelewa wako na kasumba ndio iliyokuchanganya ,Karume ni mzaliwa wa Malawi aliwatumia manamba kutoka msumbiji na wengine kutoka Tanganyika ukimchanganya na Karume mwenyewe wote walitumiliwa kufanya mapinduzi au machafuzi ya Zanzibar na walioongoza machafuzi hayo ni vijana wa kiarabu baada ya kufanikiwa machafuzi ndio yakafanywa mapinduzi Karume akawageukia wenzake na kuwatimua kila mmoja arudi alipotoka na wale waliokuwa wenyeji wazalendo akiwabaka mmoja mmoja na kuwasokota na wengine wakizikwa wazima wazima ,hao si waarabu kama unayotaka tuone kuwa waliopinduliwa na kuondosha ni waarabu bali ni wazalendo ambao hadi hii leo waZanzibar jazaba zikiwapanda wanahoji na hata gazeti la Dira liliwahi kuandika makala za watu waliotoweka baada ya machafuzi ambao walikuwa si waarabu bali ni wasomi waliobobea wakizalendo Karume alikuwa si msomi na akihofia wasomi.
Kama kurudisha utawala basi utawala unaotaka kurudishwa ni wa kizalendo na hizo damu zilizomwagika ambao unaona zimekugusa ni damu za waliokwenda kuichafua Zanzibar waliobakia karume akawafurusha ndio nyie wajukuu sasa mna uchungu wakati hamuwezi kuhji wazee wenu walikwenda kufanya nini Zanzibar.
Sasa ukielekea Pemba ambako huko hakukufanyika machafuzi sijui ni mzee wako gani mweusi aliekwenda kuwaondosha waarabu wa huko na alifanikiwa au alipigana na waarabu gani na kufanikiwa kuwaua au kuwakimbiza wangapi ?
Je wale G55 ni kitu gani kilichowasibu ? Unapowasema waPemba usifikiri kutakaliwa kimya ,kwani kama ni hatari walichokidai G55 ni kikubwa zaidi kuliko walichodai WaPemba kaa ufahamu hadi hii leo Mh.Kikwete hajaligusia na kulizungumzia jambo hilo kabisa kwani na yeye atakuwemo humo mwa Wapemba as far as all are counted as part of United Republic of Tanzania.
Kama haitoshi walipofikia G55 ni pakubwa zaidi kuliko walipofikia Wapemba na ushahidi wa madai utaona ushahidi wa Wapemba ni mkubwa zaidi kuliko wa G55 ,na hata Mchungaji Mtikila nae huzuka mara kwa mara na alisema kuwa atahamasisha WaTanganyika wadai serikali yao ,hatukusikia kukemewa wala kukamatwa au kuhusishwa na uhaini , ndugu mkuki kwa ngurue tu ? Na Mtikila hakuwa hata na saini ya mtu mmoja ni mtu aliejiamini ambae anakwenda kivyake vyake na kwa vile si suala dogo Usalama wa Taifa hatujausikia kumteka usiku wa manane ,Pemba si umesikia wamekwenda na madege ya kijeshi kama ilivyoingiliwa Entebe na Wayahudi ,Mtikila haendi kwenye UN wala kutoa taarifa rasmi lakini WaPemba wamekwenda na ushaidi kamili kuwa upindwaji wa haki zao za kimsingi kama binadamu umevuka mipaka wanasema na kuihusisha CUF so Mtikila kwani hana Chama G55 hawana Chama mbona hatukusikia kukurukakara za madegeya kijeshi na magari ya deraya kwa nini waPemba wakiwa na signature za watu elfukumi mkononi huoni kama haki zao za kimsingi zimekiukwa ,ingawa umewaona hawana akili timamu lakini kipimo ulichowapimia naona hakilingani na hoja zao ,muarabu au mkoloni gani anatamani kurudi Pemba ? Au umikusudia hawa koko tulionao mitaani ambao nao wanakula ugali kwa papa na mlenda ? Kama ulivyojaribu kusema kinachowafanya WaPemba watumie sheria kudai ni kwa ajili ya maslahi yao wao na vizazi vyao mambo ya kupigwa na kubakwa kila unapofanyika uchaguzi mkuu hawayajaona kwa kile unachokidai cha kufanyiwa wakoloni weupe bali marungu na risasi za moto huishia katika miili yao kwa kumueka mkoloni mweusi.