Polisi kuwaachia Wapemba

mkjj haya yote unayaandika saa ngapi?

mkuu nashindwa kupata picha
 
wamewaachia kwa kuwa hawakuwa na sababu za kuwakamata.
kikwete anaaibisha kuwa hawezi kutumia nguvu zake alizopewa kikatiba mpaka awasikilize wazungu.
hivi tutaendelea kutawaliwa na wazungu hadi lini?
 

Good job mwanakijiji,

Masuala ya watanzania yanaweza kuamuliwa na watanzania kwanza na sio lazima wageni watoe matamko ndio watu wakae chini kujadiliana.
 
Kaka, hii MIKUKI...

Kama wana nia, basi wamepata pa kuanzia kwa hizo point zenye meno!
 
mnanifanya niwe nervous... what is the problem.... sipendi kuandika makosa.. so you better point 'em out ili nisahihishe au niweke sawa..
...hakuna makosa mkuu, ujumbe mzito ndani ya muda mfupi ndo uliosababisha hiyo "duh..."!! Seems like all keypads are at your fingertips -- hahahh!!
 
JS, unajua mara nyingi wanatulaumu kuwa tunawakosoa tu, hatutoi mapendekezo ya suluhisho la matatizo. I hope mmoja wao atanyaka na kuongezea katika hayo. Binafsi naamini matatizo ya Pemba na Zanzibar kwa ujumla yanatatulika.
 

Asante Mwanakijiji hii nimeiweka kwenye briefcase yangu, ni hazina ya mawazo mazuri ya kizalendo, yaliyo jaa busara. Mifano ya kujitenga mingine ipo hapa hapa karibu tu, hapo Somalia. Somaliland sasa ni nchi inayojitegemea kabisa. Sasa kwanini tufike huko? kwanini mwingine ajione anaonewa ndani ya nchi yetu hii Tanzania? Viongozi na chama dola wanataka kusababisha kuvunjika kwa muungano. Nawaomba watawala watumie busara zaidi kuliko umbwamba wa kisiasa. God bless our United Republic of Tanzania.
 
Mwanakijiji,umenivutia kwa yale uliyoyaandika,ni hoja za uhakika.kam Mheshimiwa anasoma kwenye mtandao huu basi hayo mambo muhimu namshauri ayafuate ili kujijengea heshima hapa duniani.

Kina Mandela walifanya yale mambo ya msingi ya kudadi haki kwa raia na Jk anahitaji kufanya hivyo sasa....otherwise ataonekana kama wengine waliomtangulia ambao hawakutaka ku address masuala ya kimsingi ya demokrasia na haki za binadamu huko Zanzibar.
Kwa cheo chake cha Urais na kama Mwenyekiti wa AU ana mengi ya kuthubutu kufanya ili kuleta hali ya hamnazo kuondoka huko Zanzibar na tanzania kwa jumla.Sitaki Jk akawa fisadi lakini nataka kusikia muziki wa Jk mletaji amani na matumaini ya raia nchini mwetu.

Kama anaweza litakuwa ni moja ya mambo makubwa kufanyika hapa Afrika.Asipoweza....atakuwa kama mafisadi wengine tu hata kama atakuwa hajaiba BOT.
 
JS, unajua mara nyingi wanatulaumu kuwa tunawakosoa tu, hatutoi mapendekezo ya suluhisho la matatizo. I hope mmoja wao atanyaka na kuongezea katika hayo. Binafsi naamini matatizo ya Pemba na Zanzibar kwa ujumla yanatatulika.
...ni kweli kaka; tatizo la Pemba ni hicho kisiki kinachoendela kukariri kuwa Babake alifanya mapinduzi ilhali alikuwa mwoga ka' MBWA KOKO!!
 
ok.. waheshimiwa mwisho hili libichwa litagusa ardhini.. tusonge mbele tuone jinsi gani tunaweza kusaidia kutafuta usuluhishi wa mgogoro huu usio wa lazima. Kuna hatua nyingine nyingi ambazo tunaweza kujifunza kutoka nchi nyingine ambazo kwa hakika zinaweza kumaliza mgogoro huu na kufuta hata hisia za kibaguzi, uonevu, au ukandamizaji.

Kwangu mimi tatizo la mazungumzo ya muafaka ulivyo sasa ni kuwa unashughulikia dalili tu za tatizo na haugusi tatizo lenyewe. Hata mapendekezo ya kuunda serikali ya mseto na kuongeza vyeo vingine vyote vinajaribu kutibu dalili na si chanzo.

Matatizo ya mpasuko wa kisiasa hayakutokea sababu ya uchaguzi wa 95, 00, au 05. Yaliyotokea wakati huo ni ishara ya kiini cha matatizo yenyewe na mazungumzo haya ya sasa hayadeal na issues zenyewe na hivyo kuahidi kuwa mgogoro huu utaendelea kwa kizazi kingine.

Binafsi ningependekeza mgogoro uamuliwe kwa hatua. Nitafafanua kwa kirefu wiki ijayo.
 
''Amani haitafutwi kwa ncha ya Upanga...Tuliwapinga makaburu si kwa sababu ya rangi yao ila kwa dhambi ya ubaguzi wao''

Mara kadhaa imeshadhihiri njia ya kutumia mabavu haijawahi kuleta suluhusho la kudumu na la muda mrefu katika nyanja kadhaa za maisha ya mwanadamu.

Kitendo cha kuwakamata na kuwatishia wale ndg zetu wa Pemba havitaleta suluhisho la kudumu ni lazima akili na busara ya juu ifanye kazi kutatua mpasuko uliopo ktk siasa za visiwa vile vya marashi ya karafuu.

Usanii wa kupeleka maoni kwa wananchi unatia mashaka kama kweli wakulu wa chama tawala wanayo dhamira ya kweli, njema na safi ya kutaka kutafutia suluhisho la kudumu mfukuto uliopo kule visiwani. Kwani mwisho wa yote maoni yatabeba taswira ile ile ya matokea ya uchaguzi mkuu uliopita na zingine zilizopita na hapo sasa ndipo uongozi wa hali juu unatakiwa kuonyweshwa na wale wenye dhamira safi kwa kufanya maamuzi magumu yenye kuleta mwangaza mpya wa matumaini kwa Taifa mfano; Serikali ya pamoja na njia zingine zitakazokuwa muafaka kwa wakati na mazingira tuliyonayo.

Zipo pia dalili za kibaguzi kwa baadhi ya Waunguja kujiona ni bora zaidi ya Wapemba na vivyo hivyo kwa baadhi ya Wapemba kujiona wao ni zaidi. Huu ni ukaburu na ni lazima tukumbushane tuliwapinga makaburi kwa dhambi hii ya ubaguzi na si kwa sababu nyingine. Sisi ni wamoja; usawa, kuheshimiana, kuvumiliana na kutambua vipaji vya wengine miongoni mwetu ndio njia pekee ya kulea jamii ya kistaarabu na itakayokuwa na manufaa kwa wote.

Mungu Ibariki Tanzania
Ee Mungu Utulinde na maadui wa Muungano wetu.
Bara juu, Unguja juu na Pemba juu.
 
kumbe kilichotokea ni kuwa wale 10,000 walituma ujumbe leo kuwa wako tayari kwenda kujisalimisha na wenyewe Polisi ili wote watiwe pingu... ndio kisa cha kina Mwema kuwaachilia.

huko tunakokwenda jela hazitotumika tena kuzima mawazo ya kisiasa!
 
Polisi mkumbuke kwamba nynyi ndio wa kwanza kuvunja sheria na ukiukwaji wa haki za BInadamu katika kisiwa cha Pemba na kama Wapemba wamekiuka sheria na kuhusika na kuivunja Katiba basi Jeshi la Polisi linahusika moja kwa moja na washawasha la Wapemba hao.
Jeshi la Polisi linahusika moja kwa moja katika kuharibu uchaguzi wa Zanzibar sio siri kuwa jeshi la Polisi lilikuwa mstari wa mbele katika kuwalinda Janjaweeds wa Karume katika kupiga mitaa kwa zamu ,njia na mipango yote ikivuja na sehemu nyengine haari zikifika kuwa leo ni sehemu fulani ,magari yanayowachukuwa Janjaweed yakipata escort za jeshi la polisi na kuwafanya mafedhuli hao wapige wananchi kwa kutumia monyororo na nondo zikiwemo silaha zenye ncha kali.
Je ni kesi ngapi ziliripotiwa watu kupigwa na Janjaweeds na Polisi mtuambie mlichukua hatua gani ?
Je ni vituo vingapi vya kupigia kura mapandikizi walikuwa wakishushwa na magari ili kupiga kura na jeshi la polisi likiwawekea ubavu ili wapige kura haraka na kupelekwa kituo kingine ,picha za kideo zipo zinzoonyesha watu hawa ,kuna kituo kimoja janjaweed alikamatwa na kisu na baada ya kukurupushwa polisi walimuekea ubavu na kumtorosha na hakuna alilofanywa kaseti ya kideo ipo.
Je ile kesi ya Polisi kukimbia na masanduku ya kupigia kura kule Pemba ,kama si kuiba uchaguzi ilikuwa ni kitu gani ,sasa mnataka Wapemba na Waunguja wawaamini kwa jambo gani ?
Wapemba na Waunguja waseme mara ngapi hawana imani na jeshi la Polisi ?
Je mmewapa jibu gani kurudisha imani au huko kuwakamata Wapemba usiku ?
Raisi anaposema kuwa Jeshi la polisi linatakiwa kuwa karibu na wananchi ili liweze kukubalika na kubadilika hamaanishi mjiweke karibu na vyama vya siasa na kukingia kifua upande mmoja wa Chama kwa ufupi Jeshi la Polisi linatuka na kukitumikia Kundi la wahafidhina na wapo tayari kuuwa ili kulilinda kundi hilo na ndio kilichofanyka katika mauaji ya January 2001.
Polisi lilikimbia na masanduku ya kura ili kulilinda kundi hilo.
Polisi waliwazingira wafuasi wa CUF pale makao makuu yao ili kulilinda kundi hilo kuhalalisha wizi wake wa kura.
Polisi walisaidia kuruhusu wapiga kura wapandikizwaji ili kulilinda kundi hilo.
Polisi ni watumiliwa wakubwa na walioko mstari wa mbele kwa kuvunja sheria na haki za Binadamu.
Polisi walitumiliwa kuweka road Blocks na kuwasachi wafuasi wa CUF kila wanapoelekea kwenye mikutano yao na wakiwasachi na kuwavua nguo.
Jeshi la polisi lilitumika kuwatesa wakamatajwi waliopinga mapandikizi katika vituo vya Uchaguzi.
Jeshi la Polisi linatumika kwa mara nyengine kuwakamata Wapemba abao kwa kutumia kitengo cha haki za Binadamu wamewakilisha madai yao ya kujitenga kwa kule kuona kuwa hawatendewi haki na Serikali zote mbili kama wao si Raia wa Nchi hii ,hivyo imetaka UN iliangalie hili na ukiwepo uwezekano wa wao kuanzisha serikali yao basi waruhusiwe maana wametengwa kwa kila kigezo.
Kuwaachilia watu hawa sio mwisho wa mapigano dhidi ya Udhalilishaji wa jamii ya watu wa Pemba huko kwao huu ni mwanzo mpaka kieleweke kwa watawala weusi kukaa sawa na kuheshimu wenzao weusi.
 
Habari za kuaminika zinasema bado hajaachiwa mtu.
hajakabidhiwa mtu bado wapo katika vyombo vya ulinzi na usalama na wao wenyewe eti ndio watakaowasafirisha kuwapeleka Pemba ingawa hadi sasa bado hawajapelekwa licha ya kuachiwa huru tokea asubuhi.
Ilikuwa rahisi kuwateka nyara lakini baada ya kuona wamekwenda mchomo na gea waliyoondokea ,eti sasa usafiri wa kuwarudisha hawana Je huu ni Uungwana ??
 
Mwibaaaa
Tunawalaumu hao polisi lakini lazima tujue kwamba hao wanafuata maelekezo ya wakubwa wao ambao wana hasira na harakati zoote za kupelekea kukosa mlo
Kama ksura kikwete alikuwa hayataki hayo basi wala yasingeli fanyika na kutia aibu taifa [ingawa wao hawaiyoni]
Sisi wazee wetu walituachia urithi wa Kumushemu mtu mzima [makamo] kunamsemo hata muumba wa vyoote anamuheshi mtu mzima hivi kweli katika hicho kikundi chenu akina kisura hakuna hata mmoja anaye yafahamu haya? hamuelewi kama hakuna maisha ya milele hapa duniani?wakati kila siku munahudhuria mazishi?yuko wapi Swahiba DITOna wengineo wengiii
hpa dunaia tuna pita kudhalilisha hakuna maana hao wazee wa watu kama mauti yata wafikia huko waliko ninimutajitetea?
jee wale walio peperusha vikaratasi ya kuwa Wapemba warudi kwao walichukuliwa hatua gani na jeshi la polisi au polisi imesema nini kuhusu hilo?
Inamaana ni zuri kwa watawala na wanalipenda khaaswa Lakini la hawavibabu wa watu ni uhaini mimi nina uhakika mkubwa kwamba vile vikaratasi vinge andikwa kuwa 'wa bara warudi kwao' serikali zooote zingeli kemea kwa uchungu saana
eeemungu kila ajae na shari
waijuayake siri
ivunjeyake dhamiri
asiweze kusimama
mungu ibariki tanzania.
 
Jamani Mimi Namshangaa Mwema; Huyu Mwanasheria Tena Wa Kusomea na mwenye shahada Kufanya Makosa ya wazi wazi hivi.
Hawa Wapemba Walifanya Kosa Lipi La Kuvunja Katiba? Wao Hawajavunja Muungano Wala Kutangaza Serikali Yao Mpya; Hapana; Wao Walichofanya Ni Kuomba Umoja Wa Mataifa Uingilie Kati Ili Wao Wawe Ni Serikali Ndani Ya Serikali Kama Inavyotokea Katika Nchi Zingine. Na kwa kweli walikuwa na hoja katika hili.
Shida Ya Serikali Yetu Ni Baadhi Ya Viongozi Wetu Ambao Wao Wanadhani Maamuzi Yao Ndiyo Final Hata Kama Watanzania Wote Watakuwa Hawayapendi.
Wanapozungumzia Katiba Wanajisema Wao. Wanamaana Ya Matumbo Yao. Wana Maana Familia Zao. Wana Maana Rafiki Zao. Hiyo kwao ndiyo Katiba.
Ndiyo Maana Tunahitaji Katiba Mpya.
Hii Katiba Inayotukataza Hata Kuja Na Hoja Hatuitaki.
Mwema Alifanya Makosa Na Bila Shaka Alifanya Makosa Kwa Kutumwa Na Wakubwa Wake Huku Akijua Ni Makosa.
Ni Makosa Haya Haya Aliyafanya Wakati Akiingilia Masuala Ya Jf Na Kuwakamata Wale Vijana Wawili. Aliishia kulalama na kuomba radhi.
Mimi Namshauri Mwema Akamate Wale Mafisadi Wa Epa Kwanza; Na Wale Wa Richmond; Meremeta; Na Huyu Balali; Si Anajua Kuwa Wamevunja Katiba? Kwa Hawa anasemaje? Mbona Kwa Kujifanya Ni Mtaalamu Wa Interpol Kashindwa Kumpata Balali Na Kumrudisha Kujibu Tuhuma Zake za wizi?
Wapemba hawana kosa awaachie huru na awaache walete hoja hata kama ni UN. Yawezekana wamegundua wakiileta mbele ya wanafiki hawa wa CCM hawatasikilizwa.
By the way hivi kwa hili wanadhani watawanyazisha? Subirini tuone!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…