Polisi: Malisa alikamatwa akiwa na mwenzake kutokana na tuhuma za jinai

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema lilimkamata Godlisten Elisante Malisa akiwa na mwenzake usiku wa Agosti 31, 2026, kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zikichunguzwa dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Malisa na mwenzake walifanyiwa mahojiano na Jeshi hilo kufuatia tuhuma hizo.

Polisi imesema baada ya mahojiano, Malisa na mwenzake wameachiwa kwa dhamana huku wakisubiri taratibu nyingine za kisheria kukamilishwa.

Taarifa hiyo ya Polisi imekuja baada ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kutoa wito kwa Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kueleza mahali Malisa alipokuwa akishikiliwa na sababu za hatua hiyo.

 
Siku hizi Msumbiji kuna kosa jipya linaitwa Jinai?,me nlidhani labda jinai ni kundi la makosa fulani ambayo kwa ujumla wake yanaitwa jinai kama jinsi ambavyo mahindi,mchele,mtama,uwele na soya kwa pamoja ni nafaka!
 
Daah kaka ana nondo kule instagram...anasaidia watu kwny page yake...inshort ni muadilifu
Mungu atapambana na watesi wake
 
CCM ukiwa zidi akili tu lazima wakuwekee shuruba yoyote ili usiwe free! Nendeni mkasome na nyinyi harafu tumieni elimu zenu ipasavyo sio kurudi kuwa machawa. Hapo utakuta wamemwelekeza afanye nini ili asiwabuguzi! Aibu utaona wewe
 
Ni kweli kabisa, habari za nchi nyingine zikitufanya tuamini wananchi wa nchi zile ni watu wa hovyo bila kujua undani wa matatizo yao na yale waliyokuwa wanakabiliana nayo. Ndiyo maana tunaambiwa kwenye maisha tusihukumu mtu kabla hatujajua anayopitia.
 
Jinai gani?...

Kwanini hawakutoa taarifa jinai inayomkabili ili aende kituoni mwenyewe?

Yaan upotee na mtu saa 8 kelele zimezidi na kwakua mlirekodiwa ndio mnajidai ni jinai?
 
Wewe upo wapi ndugu!
Soma thread nyingine kabla ya kupost.
 
Kuna kazi zinamhitaji mtu kujitoa ufahamu ndipo atafanikiwa kuzifanya. Mimi nisingeweza kabisa kuwa polisi kwenye hii nchi.
 
Mtuhumiwa mwenyewe anadai alisindikizwa kulala chuo cha diplomasia.

Kwahiyo waliotoa hiyo taarifa wanadanganya uma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…