Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi mkoa wa Mara linamshikilia Dickson Juma umri miaka 32,mzanaki na mkazi wa Kiabakari wilayani Butiama kwa tuhuma za kuingia bila kibali na kufanya fujo katika kituo cha afya cha Nyasho kilichopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Tukio hilo limetokea Septemba 09,2026 majira ya saa 04:00 asubuhi baada ya mtuhumiwa huyo kufika kituoni hapo akitaka kuwaona mke na mtoto wake waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo licha ya kuwa muda wa kuona wagonjwa ukiwa umekwisha.Baada ya kuzuiliwa na walinzi na kutakiwa kufuata taratibu za kituo hicho mtuhumiwa alianza kufanya fujo,kuvua nguo zote na kisha kupanda juu ya mlingoti wa bendera ya taifa kama njia ya kushinikiza kuruhusiwa kuingia ndani kuona familia yake.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
Wito
Jeshi la Polisi mkoa wa Mara linatoa wito kwa wananchi kuheshimu sheria,kanuni na taratibu za taasisi za umma.