Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Polisi Kata ya Uyole Jijini Mbeya, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Charles Buyuya amewataka Maafisa Usafirishaji wa Stendi ya Makasini Uyole Junction kuwa mabalozi wa Amani katika maeneo yao.
Wito huo ameutoa Juni 25, 2026 wakati akizungumza na Maafisa Usafirishaji hao ambapo aliwasisitiza kutojihusisha na mikusanyiko isiyo rasmi na endapo kuna wito wowote wa mkusanyiko wafuatilie kupata uhalali wa mkusanyiko huo ili kuepuka mkono wa sheria.
Soma Pia: Polisi Tarime: Bodaboda dumisheni na kuilinda amani ya nchi hii
Aidha, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Buyuya amewataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani, uhalifu na wahalifu ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria ili kutokomeza vitendo hivyo