Polisi Mbeya wamnasa mwizi wa ng’ombe, mwingine aponzwa na Bangi

Polisi Mbeya wamnasa mwizi wa ng’ombe, mwingine aponzwa na Bangi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kuzaga 2.JPG

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika muendelezo wa misako inayofanyika katika maeneo ya Mkoa wa Mbeya, linamshikilia Hewad Jackson (33), Mkazi wa Kijiji cha Ilembo Mbeya Vijijini kwa tuhuma za kupatikana na ng'ombe 10 wa wizi wenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano [15,000,000/=].

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amebainisha awali mnamo 02.03.2023 huko Kijiji cha Ntokela kilichopo Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilimtilia mashaka mtuhumiwa baada ya kumuona akiwaswaga ng’ombe 10.

Alipokamatwa na wakati akiendelea kuhojiwa katika ofisi ya Kijiji cha Ntokela alijitokeza mhanga aliyeibiwa ng’ombe zake aitwaye Thadeo William (50) Mkazi wa Kijiji cha Shango ambaye alizitambua ng'ombe hizo kuwa zimeibiwa huko kijiji cha Kikondo kilichopo Kata ya Ilungu Mbeya vijijini.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa ili kujua watu anaoshilikiana nao katika matukio ya wizi wa mifugo Pamoja na kujua maeneo anayouza ng’ombe hao.

Bangi yamponza Filimoni Lambasika
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia FILIMONI LAMBASIKA [38] Mkazi wa Sambilimwaya Wilayani Chunya kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bhangi kiasi cha debe nne yenye uzito wa kilogramu 15.

Mtuhumiwa alikamatwa Machi 02, 2023 majira ya saa 07:30 mchana katika msako uliofanyika huko Kitongoji cha Sambilimwaya, Kijiji cha Chokaa, Wilaya ya Chunya. Mtuhumiwa alikamatwa akiwa anafanya biashara ya kuuza dawa hizo za kulevya akiwa ameifunga kwenye mifuko ya nailoni alimaarufu rambo na mfuko wa sandarusi.

WITO:
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amesema “Tunatoa wito kwa wananchi kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na vipodozi vilivyopigwa marufuku nchini vyenye viambata sumu kwani ni hatari kwa afya zao.

“Pia tunatoa wito kwa yeyote aliyeibiwa ng’ombe, kufika kituo cha Polisi Tukuyu Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya utambuzi wa mifugo yake.”
 
Back
Top Bottom