Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva aitwaye Said Rajab [35] mkazi wa Dar es Salaam aliyekuwa akiendesha Gari yenye namba za usajili T.422 AKF/T.303 APW Scania Lori mali ya Amani Uledi wa Moshi baada ya kusababisha ajali iliyopelekea majeruhi watatu.
Ajali hiyo imetokea Mei 06, 2024 majira ya saa 7:30 mchana eneo la Mbembela Jijini Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya – Songwe wakati Gari hilo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Zambia likiwa limebeba Mchele kuacha njia, kupinduka na kugonga Pikipiki aina ya TVS ambayo namba yake ya usajili bado kufahamika kutokana na kuharibika iliyokuwa ikiendeshwa na Ambakisye Ruben Kyejo [41] mkazi wa Chunya.
Katika ajali hiyo watu watatu wamejeruhiwa akiwemo Dereva wa Lori hilo, aliyekuwa Dereva wa Pikipiki Ambakisye Kyejo na aliyekuwa tingo wa Lori hilo Kasim Hussein [22] mkazi wa Dar es Salaam ambao wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa Gari T.422 AKF/T.303 APW Scania Lori kushindwa kulimudu Gari kwenye eneo lenye mteremko mkali. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva kuwa makini hasa katika maeneo yenye milima na miteremko mikali ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Imetolewa na:
Abdi Issango – SACP
Kaimu Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.