Mkutano huu ulikuwa uhutubiwe na Zitto Kabwe, kesho Septemba 21, 2024 pia wamezuia mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara, Isihaka Mchinjita aliyekuwa afanye ziara na mkutano wa hadhara katika Jimbo la Kinondoni.
Viongozi wa ACT Wazalendo walianza ziara ya kuzunguka mikoa tofauti nchini kuanzia Septemba 11, 2024, ziara ilitarajiwa kumalizika Oktoba 4, 2024.