tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Jeshi la Polisi mkoani Manyara, linamshikilia mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boay wilayani Babati, Eleth Mtaita akidaiwa kufanya uchochezi.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi leo Jumamosi Oktoba 25 mwaka 2025, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani amesema mchungaji huyo hakutekwa, bali alikamatwa jana Oktoba 24 mwaka 2025 na wanamshikilia kwa mahojiano kuhusu tuhuma za uchochezi.
Soma pia: Mchungaji Elieth Eliawaha Mtaita wa Kanisa KKKT Babati vijini ametekwa na watu wasiojulikana
"Huyo mchungaji hajatekwa, Polisi tunamshikilia tunamuhoji kwani anafanya uchochezi kwenye kanisa lake kuhusiana na watu wasiende kupiga kura," amesema Kamanda Makarani.
Amesema pia wanamtafuta mmoja kati ya masheikhe wa msikiti uliopo eneo hilo la Boay, Juma Silima pia kwa kuwataka watu wasiende kupiga kura Oktoba 29 mwaka 2025.
Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuendelea kuzungumza juu ya masuala ya kumuabudu Mungu na si kujihusisha na mambo ya siasa.
"Kanisani na msikitini si mahali pa kufanya siasa, hivyo tunamshikilia mchungaji huyo na pia huyo sheikh tunaendelea kumtafuta kwa kufanya uchochezi," amesema Makarani.