tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kikiendelea kudai wanachama wake 10 kushirikiliwa na Polisi Mkoa Pwani, pasipo kutoa haki ya kuonana na mawikili wao, jeshi hilo limesisitiza waliokamatwa ni wahalifu siyo makada wa chama hicho.
Kwa mujibu wa Chadema, imedai kuwa polisi liliwakamata wanachama wake sita jana Jumamosi Agosti 16, 2025 waliokuwa na kikao cha ndani Kibaha mkoani Pwani.
Miongoni waliokamatwa ni kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar es Salaam kuwa ni Pendo Msechu, Pendo Kyosi, Mary Mushi, Samson Mzambia, Focus Laurent na Alfred Bundala.
Hata hivyo, Agosti 17, 2025 Polisi mkoani Pwani ilitoa taarifa kwa umma ikisema imewakamata watu 10 waliokuwa Ukumbi wa Mwitongo Kibaha Mailimoja Shule wakipanga njama za kufanya uhalifu.
Leo Jumanne Agosti 19, 2025 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia ametoa taarifa kwa umma, akidai polisi imewazuia makada kutoonana na mawakili wala ndugu zao.
Wakati Rupia akieleza hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase amesema “Waulize wao (Chadema) walikutana na nani? Maana mimi sijakamata mtu wa Chadema. Nimekamata wahalifu sawa brother (kaka), hiyo ya Chadema waambie wakamuulize mtu anayehusika na vyama vya siasa,”amesema Morcase.