Polisi mmeshindwa kazi

Polisi mmeshindwa kazi

kambitza

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2013
Posts
2,045
Reaction score
1,320
Kwa machungu niliyoyapata ilinibidi nikae kimya bila kusema chochote, nimeugulia kipindi chote maumivu ambayo naamini kabisa yamesababishwa na utendaji kazi mbovu wa Jeshi letu la polisi nchini ambalo ndilo lenye jukumu la ulinzi na usalama wa watu na mali zao.

Kwa watu wa kijitonyama hasa maeneo ya kuanzia shule ya msingi Kijitonyama, Akachube, Bwawani Street na makumbusho, wiki mbili hizi kumeshuhudiwa matukio ya kihalifu ambayo si tu yameacha gumzo, bali yametia wasi wasi na woga kwa wakazi wa maeneo haya.

Wahalifu wanafanya kazi yao bila wasi wasi, Wanafanya watakavyo muda wowote wautakao, maduka si chini ya manne yameshavamiwa hadi sasa
Majambazi yanakusanya mauzo ya kila duka siku baada ya siku, huu mchezo ni endelevu hapa tumekaa tunasubiri kujua leo ni zamu ya nani.

Wizi wa magari sasa!!. Umeshamiri kiasi kwamba wamiliki wanatamani wapande nayo kitandani, inasemekana wapo watu wananua magari kwa walinzi gari mbili milioni 4 mbinu wanazotumia ni kupanga na walinzi siku ya tukio mlinzi anapewa kinywaji chenye madawa huku akijua mchezo mzima, kukicha mtaamsha mlinzi weee hadi mjute. Kitakachofata ni kumpeleka hospital huku mkiamini amenyweshwa madawa bila kujua.. kumbe ni danganya toto anajua kila kitu magari yote yanaibiwa hivyo ni mbinu ambayo wezi wa magari huku kwetu wamekuwa wakiitumia.

Wizi mwingine ni wavifaa vya magari yaani ile umeamka asubuhi unakuta sio gari tena ni kama chuma chakavu.
Wamefungua kila kitu hili ndiyo limenikuta mimi, wamepanda ukuta wamefanya kazi yao bila wasiwasi wowote wakaondoka zao, nimeamka asubuhi nikaona hayo niliyoyaona.

Kinachoniuma ni namna ambavyo polisi hasa wa kituo cha mabatini wanavyoyachukulia matukio yote haya, taarifa za matukio yote haya wanazo... chakushangaza sioni dalili zozote za kuyashughulikia wapowapo tu na bado matukio yanaendelea hii inaendelea kutufanya kuendelea kukosa imani na watu wenye dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu. Wezi wanajulikana, maeneo vinapouzwa hivyo vitu baada ya kuibiwa yanajulikana sasa kinachowakwamisha kuchukua hatua ni nini??

Baada ya kuibiwa nikatoa taarifa polisi walichoniambia ni kuwa wanafuatilia nilipoona kimya nikaingia mtaani vinapouzwa mfanyabiashara mmoja bila woga ananiambia nisiwafuatilie nikijitia kimbembele watakuja kuchukua na matairi yaani gari yangu itakuwa juu ya mawe Heeee!!.. viburi vyote wanatoa wapi?? Inasemekana baadhi ya polisi wasiowaaminifu wanakula nao!. Wana mgao katika kila tukio ndomana ulinzi haupewi nguvu.... kama ni hivyo tumekwisha.

Afisa upelelezi wilaya ya kinondoni mwamshe wa mabatini mwambie hatuna amani kijitonyama na wezi anawajua na kama nyote mmelala tunaomba yoyote mwenye mamlaka afanye kazi hii maana tunaishi bila amani.

Maana hadi sasa mambo yanavyokwenda inaonekana kama mmeshindwa kazi na kuwaacha wahalifu watambe.

Mwisho: sijawahi kuleta uzi humu jamvini hata siku moja. ilinibidi leo nihangaike hadi na mimi kilio changu kisikike naamini kwa kupatumia hapa kitafika.. mnisamehe kama kuna makosa makosa kiuandishi. Maji yapo shingoni.
 
Pole sana mkuu, hiyo mbona kawaida,ila Wafanyabiashara wa Spare ndio wanaosababisha yote!!!!
 
Kover yupo busy na vodacom,,,,anasisitiza matumizi ya m-pesa,,,,
 
Polisi me siwaamini kwa muda mrefu sana,,,,so wewe chukua sheria mkononi,,,,,..................:
 
amani hakuna mitaani huku
 
Pole sana hao ndo polisi wetu

Dawa ni mtaani mshirikiane mumkamate angalau mwizi mmoja awe mfano kwa wengine

Au muungane mwende mkamwone kova mwenyewe
 
Mtaani kwetu kuna ulinzi shirikishi! Walijikusanya polisi/wanajeshi/mgambo wastaafu na walioachishwa kazi kwa sababu mbalimbali na kuanzisha kakikundi kao ka ulinzi wa mitaa...kwa mwezi kila nyumba inalipa sh. 5000! Vijana wako vizuri! Nadhani mnaweza kujaribu mbinu hii kama mtaona inafaa badala ya kuilalamikia Polisi kila siku huku mkiwa wahanga wa matukio!
 
Kweli aiseee inaweza kusaidia.... lakini wajibu wa polisi unabaki palepale
 
Polisi wachukulie kama wakala wa Ulinzi na unaoita usalama wa watu na mali zao! Kama unatambua kidogo umuhimu wa bima nadhani utaniielewa...Wengi wanaweka bima kwenye mathalan magari,si kujiweka safe wakiibiwa,wakipata ajali,au wakisababisha ajali bali ili wasikamatwe na Polisi kwa kutoweka sticker. Jukumu la kujilinda lianze na wewe,na sisi!
 
Back
Top Bottom