Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,898
- 40,547
Jana aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha alikabidhi ofisi kwa Mkuu mpya wa mkoa huo Juma Homela. Moja Kati ya mambo muhimu aliyomtahadharisha ni tukio lililowahi kumtokea yeye la kutongozwa kwa njia ya simu na binti aliyemtaja Kwa jina moja la Sophia. Akifafanua Jinsi alivyolimaliza suala hilo la mtongozano alisema alilazimika kumripoti Sophia Polisi akakamatwa ndo ukawa mwisho wa kumtamani na kumsumbua kwamba anapenda kimapenzi.
Labda Polisi Tabora mtusaidie, Sophia alitenda kosa gani kuonyesha hisia zake Kwa Paulo Chacha Hadi mumkamate? Ni kifungu kipi kinasema ni kosa mwanamke kumtongoza mwanaume?
Watu wakisema CCM na Polisi lenu moja kubambikia wananchi kesi mnajitenga kama hamfahamiani lakini huu ni ushahidi tosha kiongozi wa mkoa ambaye ni mjumbe wa Kamati ya siasa mkoa ya CCM kushitaki raia tena mwanamke kwa kosa lisilokuwepo na bado Polisi wakachukua hatua kama alivyotaka Mkuu wa mkoa.