Polisi: Mnawachekea sana boda boda ipo siku watakuja kuleta maafa makubwa

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
9,024
Reaction score
18,683
Salaam

Hawa jamaa siku hizi wanapenda sana kuchukua sheria mkononi ,jioni hii kuna gari ndogo Carina Ti iligonga boda boda sijajua ni bahati mbaya au vipi basi jamaa wakaanza fujo kiasi cha kwamba dereva ilibidi akimbie na gari ,,,,,isivyo bahati wakaikamata vingunguti wakaishambulia sana ile gari huku wakiambizana wapige moto ile gari haitamaniki kwa uharibu ,sijajua maisha ya dereva.

Hii tabia imekua nguli sana hata kama umegonga kwa uzembe wao na ukataka kuonesha uungwana utoe msaada tegemea kupata ulemavu au kifo. Vijana wana hasira kali sana hii tabia ikiendelea ipo siku itagharimu maisha ya mtu mkubwa .
 
Nilipanda bodaboda Toka makumbosho 2 HQ akanipisha taa ziso zetu nikahamaki sana. Majibu yake Sasa. Bro unaogopa? Huyo nilishamalizana naye hanisbui Tena Leo. Nilishowa Cha kusema
 
Kuna mwaka fulani nje ya uwanja wa taifa kuna gari ilikuwa inarudi nyuma boda sujui alipotokea akajichomeka palepale akakata moto,ghafla wenzake wakaja wanataka kumshambulia dereva na gari,tukasimama kidete pale tukawaambia hapa haguswi mtu waka gari kuharibiwa,tukawaambia yeyote ambaye hajipendi arushe hata jiwe aone wakasanda wenyewe.
 
Shida wenye magari wanawaona Boda boda ni mbuzi.
Na boda boda wanawaona wenye magari ni ng'ombe.
Hao wote Wana waona watembea Kwa miguu ni mbwa.
Mnapita rafu rodi.unashangaa gari au boda boda inakufuata Kwa mbele yaani wanataka wewe uwapishe.kupita kati kati hawataki.
 
Mimi boda wanakuja wenyewe kwenye ngao ya Chuma nawakwepa sana wengine nikiona hawezi kumaliza kama tunapishana na gari mbele nasimama kabisa bila hivyo wangegonga sana hili Chuma na naona kabisa hawapendi maisha yao aisee kwa michezo wanayofanya mbele ya magari..
 
Bodaboda ni washenzi sana na ni wahuni. Hawa wahuni kusababisha ajali hawaoni shida. Bodaboda unampisha apite barabarani lakini atakufuata upande uliko. Wakishagonga huwa wanakimbia na kupotea hutawaona na kujua wamekimbilia wapi
 
Hii tabia imekua nguli sana hata kama umegonga kwa uzembe wao na ukataka kuonesha uungwana utoe msaada tegemea kupata ulemavu au kifo. Vijana wana hasira kali sana hii tabia ikiendelea ipo siku itagharimu maisha ya mtu mkubwa .
Uendeshaji mbovu mimi juzi hapa bila umakini wangu wangeniua barabarani au wangeniacha na ulemavu, jamaa wanaendesha vibaya sana siku hizi hususani nyakati za jioni na usiku wanaendesha vibaya mno
 
Kwanza inajulikana wazi waendesha pikipiki ni wahuni. Nchi kama Marekani pikipiki huendeshwa na magenge ya wahuni na wahalifu wakubwa. Huku madongokuinama ndio tumefanya pikipiki ndio usafiri wa chapchapu na kuwapa heshima waendesha pikipiki kwa kuwaita maofisa usafirishaji! sijui huo uafisa usafirishaji waliusomea chuo gani mpaka wakawa na ofisi zake zaidi ya kuwaona vijiweni tu
 
Nimesema hivyo kwasababu hawa wanasubiri madhara yawapate wakubwa au mtu maarufu ndo wanachukua hatua.
Mkuu ni hatua gani unataka zichukuliwe? Hili ni ''jeshi'' lililotengezwa na CCM kwa sababu ya uongozi mbovu. Hatua za kuchukuwa zinahitaji commitment ambayo hakuna kwenye utawala haramu wa sasa. The only solution ni uongozi bora. Kudhani kuwawekea sheria au kuwapiga marufuku kutasaidia ni kujidanganya.
 
Salaam

Hawa jamaa siku hizi wanapenda sana kuchukua sheria mkononi ,jioni hii kuna gari ndogo Carina Ti iligonga boda boda sijajua ni bahati mbaya au vipi basi jamaa wakaanza fujo kiasi cha kwamba dereva ilibidi akimbie na gari ,,,,,isivyo bahati wakaikamata vingunguti wakaishambulia sana ile gari huku wakiambizana wapige moto ile gari haitamaniki kwa uharibu ,sijajua maisha ya dereva.

Hii tabia imekua nguli sana hata kama umegonga kwa uzembe wao na ukataka kuonesha uungwana utoe msaada tegemea kupata ulemavu au kifo. Vijana wana hasira kali sana hii tabia ikiendelea ipo siku itagharimu maisha ya mtu mkubwa .
waache waendelee ipo siku wataingia choo cha kike.
 
Bodaboda ni washenzi sana na ni wahuni. Hawa wahuni kusababisha ajali hawaoni shida. Bodaboda unampisha apite barabarani lakini atakufuata upande uliko. Wakishagonga huwa wanakimbia na kupotea hutawaona na kujua wamekimbilia wapi
Ku-deal na bodaboda ni ku-deal na dalili za ugonjwa badala ya chanzo. Wahuni ni watawala waliofanya bodaboda iwe sehemu ya kuficha udhaifu wa uongozi mbovu.
 
Bodaboda ni washenzi sana na ni wahuni. Hawa wahuni kusababisha ajali hawaoni shida. Bodaboda unampisha apite barabarani lakini atakufuata upande uliko. Wakishagonga huwa wanakimbia na kupotea hutawaona na kujua wamekimbilia wapi
Watumiaji huwaita BODABODA.
wenye magari huwaita WAHUNI/WASHENZI
serikali huwaita MAAFISA USAFIRISHAJI.

Yote kwa yote Mungu awalinde wapambanaji wote,kwani wanategemewa.
 
Mimi kwenye gari natembea na jijisu maana sio kisu kidogo sasa mtu aniletee zake ohooooo tukutane wodini au polisi
 
Mimi boda wanakuja wenyewe kwenye ngao ya Chuma nawakwepa sana wengine nikiona hawezi kumaliza kama tunapishana na gari mbele nasimama kabisa bila hivyo wangegonga sana hili Chuma na naona kabisa hawapendi maisha yao aisee kwa michezo wanayofanya mbele ya magari..
Madereva tujaliane maisha na huu ndiyo udereva uliokamilika kuwajibika hata kwa makosa ya wengine,maisha yangekuwa bora sana kama tungekuwa tunawajibika kama hivi kwenye makosa ya wenzetu.

Hakuna mtu anayestahili kufa kama kulikuwa na uwezekano wa kufanya asife,Kongole kwa hilo mkuu
 
Watumiaji huwaita BODABODA.
wenye magari huwaita WAHUNI/WASHENZI
serikali huwaita MAAFISA USAFIRISHAJI.

Yote kwa yote Mungu awalinde wapambanaji wote,kwani wanategemewa.
serikali inawaremba kwa kuwaita maafisa usafirishaji kwa sababu inajua kabisa wale ni wahuni na ni washenzi, kukinukisha ni dakika moja tu, ni kitisho kikubwa kwa serikali, kwa hiyo inabidi serikali iwachekee na kuwabembeleza wahuni hao!
 
Back
Top Bottom