Polisi - Morogoro wathibitisha watu wawili wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Polisi - Morogoro wathibitisha watu wawili wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2025-01-30 at 12.49.08_31880bb9.jpg
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linathibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili kwa athari za maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Vifo hivyo vimetokea katika nyakati na maeneo tofauti.

Tukio mojawapo limetokea usiku wa kuamkia Januari 30, 2025 katika mtaa wa Majengo mapya, kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Hashim khasimu Juma (43), mkulima na mkazi wa kihonda B alikufa maji alipokuwa anajaribu kuvuka mto ambao ulikuwa umejaa maji kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro.

Tukio lingine limetokea Januari 29, 2025 mchana huko katika mtaa wa Mafisa, kata ya Mafiga, Manispaa ya Morogoro, umepatikana mwili wa mtu mmoja mwanaume, anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 35-40 ukiwa ndani ya maji yaliyotuama mithiri ya dimbwi akiwa tayari amefariki. Mtu huyo hajaweza kufahamika na inadhaniwa kuwa alishindwa kujiokoa baada ya kudumbukia ndani ya shimo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa kiasi kikubwa. Mwili huo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kutoa nafasi kwa ndugu kuutambua.

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linatoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kubwa wakati huu mvua zinazoendelea kunyesha. Wanashauriwa kuacha kujaribu kina cha maji kwa hisia au kwa miguu badala yake wapite kwenye maeneo au vivuko vyenye usalama.

Imetolewa na;
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Morogoro
 
Back
Top Bottom