Polisi: Mwanamke aliyerekodiwa akimpiga Mwenzake, hatua za Kisheria zitachukuliwa

Polisi: Mwanamke aliyerekodiwa akimpiga Mwenzake, hatua za Kisheria zitachukuliwa

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tangu picha mjengeo wa tukio linaloonyesha mwanamke mmoja akimpiga mwenzake ilipoanza kusambaa, ufuatiliaji umefanyika na aliye fanya kitendo hicho amefahamika majina yake, eneo analofanyia kazi na namba zake za simu.

Hatua stahiki zitaendelea kuchukuliwa kulingana na kinachoonekana kufanyika kupitia picha mjengeo hiyo sambamba na ushahidi unaoendelea kukusanywa kutoka kwa watu mbalimbali waliokuwa mashuhuda akiwepo aliyefanyiwa kitendo hicho pale atakapopatikana au atakapojitokeza.

Kwa anayemfahamu mwanamke huyo anayeonekana akipigwa amjulishwe afike dawati la jinsia Polisi Msimbazi ili hatua ziendelee kuchukuliwa dhidi ya kitendo alichofanyiwa.

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kujiepusha na tabia za kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume na sheria za nchi na hakuna aliye juu ya sheria.

snapins-ai_3748883511034831753.webp
 
Back
Top Bottom