GE2025 Polisi Mwanza Wawakumbusha Mgambo Kuheshimu Sheria Kipindi cha Kampeni na Uchaguzi

GE2025 Polisi Mwanza Wawakumbusha Mgambo Kuheshimu Sheria Kipindi cha Kampeni na Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limewataka askari wa jeshi la akiba (Mgambo) kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi hasa katika kipindi hiki cha mikutano ya kampeni na kuelekea siku ya tarehe 29 ya mwezi wa kumi ambapo itakuwa siku ya kupiga kura ya kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa ameyasema hayo wakati akizungumza na askari hao wa jeshi la akiba wa wilaya za Nyamagana na Ilemela ili kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inazidi kuimarishwa hasa katika kipindi cha kampeni na kueleka siku ya uchaguzi mkuu.

 
Back
Top Bottom