Polisi: Mwenyekiti wa BAVICHA hajatekwa bali tunamshikilia kwa tuhuma za kughushi nyaraka

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gasper Temba, hajatekwa isipokuwa amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka.

Aidha, Jeshi hilo limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika zinazoweza kusababisha taharuki.

Soma Pia : Mwenyekiti Wa BAVICHA Kanda Ya Kaskazini Adaiwa Kutekwa Na Watu Wasiojulikana
1756537973968.png

1756538019539.png

1756537539053.png

​
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gasper Temba, hajatekwa isipokuwa amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka.

Aidha, Jeshi hilo limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika zinazoweza kusababisha taharuki.

View attachment 3458975
Mangi amekatwa kwa wizi ndui life la Wachaga

USSR
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gasper Temba, hajatekwa isipokuwa amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka.

Aidha, Jeshi hilo limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika zinazoweza kusababisha taharuki.

No thank you! Namna ya ukamataji una viashiria vya utekaji
 
Wananchi watatofautisha vipi polisi na majambazi ikiwa wote wanafanya mambo yao kwa mtindo mmoja??

Kuna siku wananchi watajihami alafu mtawasababishia madhara ya bure hao constebo wenu mnaowalipa fedha kidogo.

Muda huo ninyi mkiwa mmekalisha matako yenu maofisini wakati vijana wanatiwa kibiriti na umma.

IGP komesha huu uendawazimu!
 
Ushawah kuskia mara kwa mara POLISI wanakamata watu wa CCM?
 
Kumbe huyu jamaa amekamatwa Arusha?

Nilidhani ni watu wa Dar peke yake ndiyo waoga kumbe hili ni tatizo la nchi nzima.

"Huo ujinga wa kutekana barababrani mchana kweupe huku watu wanaona ingekuwa Arusha hao jamaa tungewachoma moto wao na gari lao" .

Leo letokea Arusha/Chuga na wamerudisha mikia ndani kama wenzao wa Dar Pamoja na mikwara mbuzi yote ile.

Bado watu wa Tarime.
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gasper Temba, hajatekwa isipokuwa amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka.

Aidha, Jeshi hilo limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika zinazoweza kusababisha taharuki.

Hii tabia ya Polisi kuwakamata watu kwa njia zisizo za wazi au zinazofanania na zile za 'utekaji' inapaswa kupingwa vikali sana.
Huu ni kama uhalifu tu. Inasababisha jamii kuamini kwamba kuna uhusiano kati ya matukio ya utekaji na Jeshi la Polisi, na hivyo kupunguza imani ya wananchi kwa taasisi hii, haiwezekani taasisi yenye miongozo ya ukamataji, itumie njia sawa kabisa na zinazotumiwa na Wasiojulikana.

Kulikuwa na ugumu gani kumpa mtu wito ili ajisalimishe mwenyewe kituoni?
Ni kumnyima mtu haki ya kiutetezi na kujiandaa kidhamana....
 
Back
Top Bottom