Polisi na Magari ya Polisi wajipanga kukabiliana na CORD kesho

Hehehe, Minishi alipitia mengi.
 

Hehehe!! Pole, hapa Kenya kama hujatumia ujana wako kuhusika katika kuleta mabadiliko utakua na wakati mgumu wakati wa uzee wako.
Mimi ilinikuta siku moja nimejitokeza nikiwa kijana barobaro, kipindi cha akina Shikuku na Matiba wakati tunapambana kwa ajili ya mabadiliko. Tulipoanza mapambano na polisi halafu mabomu ya machozi yakatupwa na kulipuka, watu wakaanza kuondoka mbio. Sasa mimi kwa bahati mbaya wakati nakimbia nikajikwa na kuangukia seng'enge (barbed wire), ikanidunga mdomoni na kunibana (ilinitia kovu ambalo lipo hadi leo).

Wakati nahangaika kujiondoa, nikaona FFU wapo mbioni wananifikia, kilichoniokoa ni kwamba walikua pamoja na mkuu wao. Hivyo aliwazuia wasinipe kichapo, alinisaidia na kunikwamua kutoka hapo na kuniamrisha nitimke mbio, yaani nilitoweka kama risasi.
Yote tisa, nilihusika kwenye mabadiliko ya nchi, kama tungekua waoga waoga, leo hii tungelikua nyuma sana kwa kila kitu.

Tatizo maandamano ya siku hizi ni tofauti na ya kipindi kile, unakuta vijana wanapora na kupiga magari mawe.
 
Te te te! wee jamaa Barbarosa Kituko yaani PR kwenda mbele. Hivi ile kashfa ya binti wa Magu Jesca mumefaulu kupata pa kutokea? Naona mumekamatwa sana na Watanzania huku Mtoto wa Magufuli sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Itabidi mubuni mikakati hapo Lumumba
 
Kwa hiyo ulitakaje kwamba na sisi tuingie barabarani kama Wakenya na kuumizwa au kuuliwa na Askari kwa ajili ya Seif na Sheni?

Usisahau Seif alishasafirisha familia yake kwenda Omani kabla ya uchaguzi, records zipo!
Hahahaha. Nimependa jibu lako mkuu,
Anataka tupoteze muda wetu tuingie barabarani kisa tunataka seif awe rais.
Hawa hawa wanasiasa wanafiki wanipeleke kwa road.
Funy!!!!
Halafu Mimi huwa naamini kutumia njia mbadala ya kufanikisha haya badala ya kutumia nguvu na kupigana na police.
 
Nina jamaa yangu anaishi Kisumu, ameniambia huko kila mtu amekaa mkao wa kupambana, leo patachimbika kwenye huo mji.
 
Watanzania wamekomaaa kuuana hakuna tija mambo yote yataenda tu. Tatizo la kenya ni ukabaila tu. Kama si hilo basi mngekuwa new the first country to give grants
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…