Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Polisi wa Tanzania wameweza kutumika kwenye siasa tu , ulinzi na hasa kwenye usalama wa mashabiki na wizi wa simu na vipochi ndio wameshindwa kabisa , sisi wengine tunadhani vile vikundi vya uporaji vya uwanja wa Taifa na majirani ni vikundi vya polisi wenyewe .Mara nyingi nimekuwa naingia uwanja wa Taifa kuangalia mashindano mbalimbali ya Mpira was miguu toka uwanja wa Uhuru.
Nimeonana Mara nyingi vitendo vya udanganyifu kwa wasimamizi na pia baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi.
Kama jana wakati naingia geti la VIP B mtumishi wa selcon na Polisi walikuwa wanagombania sh 2000 aliyotoa mshabiki wa jukwaa la mzunguko ili apate nafasi VIP B
Hiyo Ni aibu kubwa Sana na matokeo yake Kuna baadhi ya mashabiki wa VIP kukosa nafasi VIP B au C kwa mfano nilimuona Lucas Mwasulama na Seif Mdangaye wakihangaika kutafuta siti zao bila mafanikio.
Na baada ya mchezo kumalizika nilipita eneo la makutano ya barabara ya Mandela na ile ya Taifa karibu na lango la Kambi ya Jeshi Twalipo hapo ndipo mashabiki walikuwa wanaporwa simu,mabegi na pochi zao mubashara yaani live na vikundi vya vijana.
Sikuamini kabisa macho yangu kwa uporaji ule huku mabinti wengi wakiwa wanalia na kukimbia ovyo happy ilikuwa ni saa moja jioni mashabiki wanaendelea kutoka uwanjani.
Kina haja mahususi kwa Jeshi la Polisi na TFF kujipanga kiulinzi zaidi kwenye mashindano ya vijana chini ya miaka 17 AFCON 2019 ktk masuala ya tiketi na jinsi kuingia uwanjani na ulinzi nje baada ya mchezo kumalizika.
Kinyume na hapo wageni wasije wakapata shida ndani uwanjani na usalama nje ya uwanja.
Huu wizi una zaidi ya miaka 10 unafanywa bila polisi kuchukua hatua zozote .