onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,356
- 1,309
Hawa polisi sasa ni dhahiri wanaingilia shughuli binafsi za mgombea wa Chadema, Tundu Lissu.
Lissu ni Mwanasiasa na shughuli kubwa kwake ni kufanya siasa. Ili uweze kutekelezwa majukumu yako kisiasa ni lazima utoke point A kwenda B kuhamasisha wanachama wako.
Uhamasishaji siyo kuomba kura bali ni kuongeza idadi ya wanachama.
Jana polisi waliingilia shughuli zake na kumzuia njiani kuendelea kwenda kutekeleza majukumu yake. Polisi walisema walitekeleza majukumu yao kwa Nia ya kumlinda.
Ni kweli Lissu anahitaji ulinzi lakini siyo kumzuia kusafiri. Au tuseme, amezuiwa kusafiri na kuonana na watu wake. Mbona sasa jeshi la polisi hatuwaelewi elewi? . Na je, wanatenda haya kwa amri ya Nani?. Mgombea wa CCM Ni rais anayeendelea lakini tofauti na kugombea {kufanya kampeni} anaendelea na shughuli za urais Kama kawaida.
Lissu ana zuio kutokufanya kampeni kwa muda wa siku 7, Sasa je, asifanye shughuli nyingine za kisiasa au kijamii?
NEC katika katazo lao walisema haruhusiwi kusimama jukwaani akifanya kampeni. Hilo Lissu na timu yake wamelitii tangu Ile trh 3, lakini kule kusafiri pia Yuko jukwaani akipiga kampeni? Unaposafiri Ni kuwa either unakuwa ndani ya gari au chombo chochote, Je, hiyo tuiite Ni kupanda jukwaani kuomba kura?
Polisi na NEC wabanwe na vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu watoe tamko kwa nini wanasakama baadhi ya vyama. Vyama vizungumze wazi na kuonya juu ya Tabia ya NEC kuwanyamazia polisi hata pale ambapo wanavunja katiba na kuvuruga mwenendo wa uchaguzi unaoendelea. Polisi na NEC wakae Kando na wasiwe washirika wa kutaka kuona mgombea wa CCM anapita bila kupata upinzani.
Mwaka huu uchaguzi ni tofauti kabisa kwa namna ambavyo Lissu alivyobadili upepo kwahiyo CCM wakubali kushindana na si vinginevyo. Waache Tabia ya kubebwa, mbona wanapowasomba watoto wa shule na kuwssitishia masomo vyama vingine havijalalamika. Wanatumia resources za serikali kwa maana usafiri pamoja na watumishi Ila vyama vingine viko tu kimya. Sasa wameanza kutumia force, polisi na NEC kuwasaidia.
Hii haikubaliki, Lissu afanye Yale aliyoelekezwa na kamwe asiingiliwe. Kwani wasiwasi wa tume na polisi Ni Nini?