Polisi Pwani: BAWACHA walikuwa wanaenda kutekeleza uhalifu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa wanachama 29 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwemo wanawake 20 na wanaume 9, ambao baadaye waliruhusiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa Machi 8, 2026 na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, wanachama hao walikamatwa Machi 6, 2026 majira ya saa 11 jioni katika eneo la Visiga, wilayani Kibaha, wakiwa wanasafiri kwa kutumia magari mawili aina ya coaster.

Polisi wamesema kukamatwa kwao kulitokana na tuhuma za kukiuka amri ya mahakama pamoja na taarifa za mipango ya kutekeleza vitendo vya kihalifu kwa kisingizio cha kwenda kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mara.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanachama hao kwa sasa wapo nje kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea na hatua zaidi za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewataka wananchi kuendelea kutii sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kudumisha amani na utulivu.

1772975937087.png
 
View attachment 3554957
tunakoelekea na haya mavyuo ya VETA ujue watu wataongeza sana uelewa kwenye kujitaftia maisha! sasa serikali inapokuja na ujinga wa kukandamiza haki hii tabia
mbaya itatoka kwenye siasa itahamia.kwenye maisha ya kawaida! itafika muda watu kuajiriiwa upolisi itakuwa kwa kulazimishwa sio kuomba wao

Mtaani hakutakuwa kunakalika kwa polisi
 
Hivi polisi mtaacha lini kujidhalilisha kwa kutumiwa na CCM kama vikaragosi? Sijui duniani kama kuna polisi wapumbavu kama polisiccm.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa wanachama 29 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwemo wanawake 20 na wanaume 9, ambao baadaye waliruhusiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa Machi 8, 2026 na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, wanachama hao walikamatwa Machi 6, 2026 majira ya saa 11 jioni katika eneo la Visiga, wilayani Kibaha, wakiwa wanasafiri kwa kutumia magari mawili aina ya coaster.

Polisi wamesema kukamatwa kwao kulitokana na tuhuma za kukiuka amri ya mahakama pamoja na taarifa za mipango ya kutekeleza vitendo vya kihalifu kwa kisingizio cha kwenda kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mara.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanachama hao kwa sasa wapo nje kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea na hatua zaidi za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewataka wananchi kuendelea kutii sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kudumisha amani na utulivu.

Hili jeshi kweli halina kazi ya maana ya kufanya. Hao walioshikwa walikua wanaenda kutekeleza uhalifu je walikutwa na silaha gani, au na maandika gani, watoe ushahidi. Kwa sababu tu ni CHADEMA basi walikuwa wanaenda kufanya uhalifu. Polisi ya Tanzania kwa sasa inaizidi hata ile ya Makaburu wa zama zile kule Afrika Kusini. Ni fedheha sana kunyanyasa Raia wa nchi hata kama wanaenda kufanya furaha yao. Huu ni unyama mkubwa sana kwa haki za binadamu.

CCM haya mnayoyafanya yatakuja kuwatokea na mtayalipa, sioni muda mrefu.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa wanachama 29 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwemo wanawake 20 na wanaume 9, ambao baadaye waliruhusiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa Machi 8, 2026 na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, wanachama hao walikamatwa Machi 6, 2026 majira ya saa 11 jioni katika eneo la Visiga, wilayani Kibaha, wakiwa wanasafiri kwa kutumia magari mawili aina ya coaster.

Polisi wamesema kukamatwa kwao kulitokana na tuhuma za kukiuka amri ya mahakama pamoja na taarifa za mipango ya kutekeleza vitendo vya kihalifu kwa kisingizio cha kwenda kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mara.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanachama hao kwa sasa wapo nje kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea na hatua zaidi za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewataka wananchi kuendelea kutii sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kudumisha amani na utulivu.

Tukisema Polisi ndiyo chanzo cha Uhalifu nchi hii muwe mnatuelewa. Polisi wamekamata Wahalifu hatari halafu wamewaachia.
 
Back
Top Bottom