Polisi Pwani Watoa Mafunzo ya Maadili kwa Waandishi wa Habari

Polisi Pwani Watoa Mafunzo ya Maadili kwa Waandishi wa Habari

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jeshi la polisi mkoani Pwani limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani humo yaliyolenga kuwaongezea ujuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo maadili.

Mafunzo hayo yaliyoongozwa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, ASP Salimu Morcase yaliangazia pia usalama kuelekea, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Sambamba na kamanda huyo pia viongozi mbalimbali wa jeshi hilo walipata nafasi ya kutoa mafunzo kwa waandishi hao ikiwemo mafunzo ya kuepuka uandishi wa hisia na upendeleo au ubaguzi kwa vyama sambamba na kuepuka kauli za chuki na ubaguzi wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi.

Katika hali ya kuhakikisha usalama wa waandishi, jeshi la polisi limewahimiza waandishi kuvaa vizibao vyenye kuwatambulisha ili inapotokea vurugu waweze kuwa salama.

Screenshot 2025-09-03 220154.png
 
Maadili ,maadili yaani mtu anagawa baiskeli na pikipiki halafu mnamwangaliaaaaaa😭😭😭
 
Back
Top Bottom