Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Dunia haiishi maajabu aiseeee. "Geshi" letu linachekesha sana kama sio kusikitisha. Anyway habari kamili hii hapa.
---
Maofisa saba wa Jeshi la Polisi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiwa na mashtaka ya wizi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh1.16 bilioni.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo Januari 10 kwa mahakimu watatu tofauti ambapo mshtakiwa Godson Kimambo na Said Shekule walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi.
Naye mshtakiwa Jane Mganga amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Luboroga.
Wengine ni Erasto Mtweve, Mahuna Kosuma, Halima Maridadi na Lameck Nyamya ambao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rhoda Ngililanga.
Wakili wa serikali, Slyvia Mitanto akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Kyaruzi, amedai kuwa mshtakiwa Kimambo na Mkue walitenda makosa yao kati ya Januari mosi mwaka 2020 hadi Septemba 30 mwaka 2021 jijini Dar es Salaam.
Mitanto amedai washitakiwa hao wakiwa watumishi wa umma kama maofisa wa jeshi hilo kwa makusudi na nia ovu waliiba zaidi ya Sh449.14 milioni mali ya jeshi hilo zilizofika kwao kulingana na nafasi zao za ajira.
Mitanto alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ambapo ilipangwa Januari 24, 2022.
Hakimu Kyaruzi amewaeleza washtakiwa hao kwamba watapelekwa rumande mpaka tarehe hiyo na kama wanahitaji dhamana wanatakiwa kuomba Mahakama Kuu yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.
Awali akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Luboroga, Wakili wa Serikali Yusuph Aboud akisoma, amedai mshtakiwa Jane alitenda makosa katika tarehe tofauti kati ya Januari Mosi, 2020 hadi Septemba 30, 2021 Ilala jijini Dar es Salaam.
Aboud amedai kuwa mshitakiwa huyo aliiba zaidi Sh488.15 milioni mali ya Jeshi la Polisi Tanzania zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya kuajiriwa.
Awali kulitokea mvutano wa kisheria baina ya mawakili wa pande zote mbili juu ya Mamlaka ya mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo na kutoa masharti ya dhamana kwakuwa kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi.
Naye Wakili wa serikali Mwandamizi, Adolf Verandomi akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu Ngililanga, amedai washtakiwa Mtweve, Kosuma na Halima walitenda makosa hayo kati ya Januari 14 mwaka 2019 hadi Septemba 15 mwaka 2021 jijini Dar es Salaam.
Ilidaiwa kwamba, washitakiwa hao wakiwa watumishi wa umma, kwa nia ovu, waiiba zaidi ya Sh212. 44 milioni mali ya Jeshi la Polisi Tanzania zilizofika kwao kulingana na nafasi zao za ajira.
Kwa upande wa mshitakiwa Nyamya ilidaiwa kati Juni 7, 2018 hadi Mei 7 mwaka 2019 aliiba zaidi ya 5.8 milioni mali ya Jeshi la Polisi Tanzania zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya kuajiriwa.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo upande wa mashitaka ulidai, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ambapo ilipangwa Januari 24, 2022.
Chanzo: Mwananchi