Polisi Tanga yanasa watu 11 wakidaiwa ni "Tuma kwa namba hii"

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Tanga. Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga likiwashikilia watuhumiwa 11 kwa makosa ya utapeli kwa njia ya mandao, majirani katika nyumba waliyokuwa wakiishi watuhumiwa hao wamesema wakiwa humo walikuwa na utamaduni wa kufungua muziki kwa sauti kubwa.

Pia wanadai watuhumiwa waliokuwa wamepanga katika Mtaa wa Donge, wakilipa kodi ya Sh800,000 kwa mwezi, walikuwa wakishi maisha ya kutotaka kuzoeana na majirani.

Wakizungumza na Mwananchi, kwa nyakati tofauti, majirani hao walidai watuhumiwa walikuwa wakitumia magari yenye vioo vya giza na pikipiki ili wasizoeleke katika eneo hilo.

Meshaki Doto, alisema kila alipojaribu kuingia kwenve nvumba hiyo kuwajulia hali, mara nyin-gi geti lilikuwa limefungwa kwa ndani.

"Kwa kawaida katika mtaa wetu huwa tunashirikiana kwa shida na raha, lakini hawa walikuwa wakiJIfungia muda mwingi na wanatoka na magari yenye vioo vilivYowekwa tinted, wanamaliza mambo yote humo humo," alisema Meshaki.

Alidai tangu walipohamia mtaa huo kati ya mwezi mmoia au miwili iliyopita, walikuwa na utamaduni wa kwenda kwenye vibanda vya kutolea pesa kwa simu.

"Binafsi nilikuwa naogopa kwa sababu nyumba hivo haikuwa ikiisha pilika za kuingia na kutoka watu wasioeleweka na hawakutaka tuingie," alidai Meshaki.

Hoja hivo iliungwa mkono na Bahati Kaniki, ambaye ni dereva wa bodaboda, aliyedai hakuwa akitambua kwamba wanaweza kuwa ni wahalifu kwa sababu usiku alikuwa akiwapeleka kwenye muziki na kuwaacha huko.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Donge, Said Karelanda alisema hawezi kubainisha mbinu zilizotumika hadi watuhumiwa hao kukamatwa kwa sababu anataka wengine wenye nia kama hiyo watambue kuwa Serikali ipo.
Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tan-ga, Henry Mwaibambe aliwataka watumiaji wa simu za mkononi kutowapa ushirikiano watu wanaowapigia simu na kuomba namba za siri.

Alisema watuhumiwa hao, wakiwamo wanawake wawili, wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za kimtandao, ikiwamo kurubuni kuwa: wanafanvia maboresho mitandao ya simu.

Alisema watuhumiwa hao 11 walikuwa wameweka kambi jijini Tanga na kuendesha wizi kwa niia ya simu katika mikoa mbalimbali. Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hadija Nyange (34), Zaina thumani (25), Innocent meme (35), Abdulaziz Nori (31), Said Hassan (24), Salum Rajab (24), Rashid Habibu (23), Said Juma (30), Idd Kaniki (35), David Rupi-ana (22) na Omary Mohamed (27).

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na simu, pikipiki, laini za simu, jiko na chetezo kwa ajili ya kuchomea laini na karatasi zene namba walizokwishatapeli na wanazotarajia kutapeli.

Pia walikuwa na fedha mbalimbali, zikiwemo Shilingi za Tanzania, Dola za Marekani na Faranga za Congo DRC.

Baada ya kuwahoji, Mwaibambe alisema walikuwa wakimtaka mwenye simu kutuma fedha na wengine kuomba namba za siri.
 
Tanga. Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga likiwashikilia watuhumiwa 11 kwa makosa ya utapeli kwa njia ya mandao, majirani katika nyumba waliyokuwa wakiishi watuhumiwa hao wamesema wakiwa humo walikuwa na utamaduni wa kufungua muziki kwa sauti kubwa.

Pia wanadai watuhumiwa waliokuwa wamepanga katika Mtaa wa Donge, wakilipa kodi ya Sh800,000 kwa mwezi, walikuwa wakishi maisha ya kutotaka kuzoeana na majirani.

Wakizungumza na Mwananchi, kwa nyakati tofauti, majirani hao walidai watuhumiwa walikuwa wakitumia magari yenye vioo vya giza na pikipiki ili wasizoeleke katika eneo hilo.

Meshaki Doto, alisema kila alipojaribu kuingia kwenve nvumba hiyo kuwajulia hali, mara nyin-gi geti lilikuwa limefungwa kwa ndani.

"Kwa kawaida katika mtaa wetu huwa tunashirikiana kwa shida na raha, lakini hawa walikuwa wakiJIfungia muda mwingi na wanatoka na magari yenye vioo vilivYowekwa tinted, wanamaliza mambo yote humo humo," alisema Meshaki.

Alidai tangu walipohamia mtaa huo kati ya mwezi mmoia au miwili iliyopita, walikuwa na utamaduni wa kwenda kwenye vibanda vya kutolea pesa kwa simu.

"Binafsi nilikuwa naogopa kwa sababu nyumba hivo haikuwa ikiisha pilika za kuingia na kutoka watu wasioeleweka na hawakutaka tuingie," alidai Meshaki.

Hoja hivo iliungwa mkono na Bahati Kaniki, ambaye ni dereva wa bodaboda, aliyedai hakuwa akitambua kwamba wanaweza kuwa ni wahalifu kwa sababu usiku alikuwa akiwapeleka kwenye muziki na kuwaacha huko.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Donge, Said Karelanda alisema hawezi kubainisha mbinu zilizotumika hadi watuhumiwa hao kukamatwa kwa sababu anataka wengine wenye nia kama hiyo watambue kuwa Serikali ipo.
Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tan-ga, Henry Mwaibambe aliwataka watumiaji wa simu za mkononi kutowapa ushirikiano watu wanaowapigia simu na kuomba namba za siri.

Alisema watuhumiwa hao, wakiwamo wanawake wawili, wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za kimtandao, ikiwamo kurubuni kuwa: wanafanvia maboresho mitandao ya simu.

Alisema watuhumiwa hao 11 walikuwa wameweka kambi jijini Tanga na kuendesha wizi kwa niia ya simu katika mikoa mbalimbali. Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hadija Nyange (34), Zaina thumani (25), Innocent meme
(35), Abdulaziz Nori (31), Said Hassan (24), Salum Rajab (24), Rashid Habibu (23), Said Juma (30), Idd Kaniki (35), David Rupi-ana (22) na Omary Mohamed (27).

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na simu, pikipiki, laini za simu, jiko na chetezo kwa ajili ya kuchomea laini na karatasi zene namba walizokwishatapeli na wanazotarajia kutapeli.

Pia walikuwa na fedha mbalimbali, zikiwemo Shilingi za Tanzania, Dola za Marekani na Faranga za Congo DRC.
Baada ya kuwahoji, Mwaibambe alisema walikuwa wakimtaka mwenye simu kutuma fedha na wengine kuomba namba za siri.
Said, human, Hasan, zuwena, Hadija, Salum, Abdul, Seleman, kassim!!! Fanyeni kazi ndugu zangu, haya madili yenu haya yanatutia aibu Watanganyika
 
Hawa wapumbavu wanatakiwa watokomezwe kabisa. Maana wanawaonea sana waanachi wasuo na uelewa wa huo utapeli wao.
 
Mmh mitaa ya Donge hakuna nyumba ya kodi laki 8 kwa mwezi! Hatua kali zichukuliwe dhidi ya utapeli huo ili iwe funzo kwa wengine!
 
Said, human, Hasan, zuwena, Hadija, Salum, Abdul, Seleman, kassim!!! Fanyeni kazi ndugu zangu, haya madili yenu haya yanatutia aibu Watanganyika
Dooohhh
 
Back
Top Bottom