GE2025 Polisi Tarime: Bodaboda dumisheni na kuilinda amani ya nchi hii

GE2025 Polisi Tarime: Bodaboda dumisheni na kuilinda amani ya nchi hii

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Miongoni mwa kundi lililopewa elimu na jeshi la polisi kipindi hichi cha uchaguzi basi ni bodaboda.

Yani sijuwi wameona kwamba ni rahisi kutumika na wanasiasa au vipi?
=================
Afisa Mnadhimu Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joswam Kaijanante amewataka maafisa usafirishaji maarufu kama Bodaboda wa wilayani Tarime kudumisha na kuilinda amani ya nchi hii.

Ametoa wito huoOktoba 17, 2025 katika kikao cha Jeshi la Polisi Tarime Rorya na Maafisa usafirishaji kilichofanyika katika ukumbi wa TTC Tarime.

Naye Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Jumanne Mkwama amewataka Bodaboda hao kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kupitia falsafa ya ulinzi shirikishi.

Screenshot 2025-10-22 235213.png
Screenshot 2025-10-22 235223.png
Screenshot 2025-10-22 235231.png
 
Boda boda wanapewa coverage karibu mikoa yote kana kwamba ni tishio, wana tishio gani wale wakati hata elimu hawana? Kila wakati bodaboda, au kwa sababu wana vijiwe? Yapo makundi mengine ambayo ni tishio kuliko bodaboda ila hayamulikwi sana
 
Mjinga ndio huwa analeta mapinduzi
Wapumbavu waliosoma wana kuwa tathmini nyingi kichwani mpaka wanageuka mafisi.....
 
Back
Top Bottom