masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,870
- 15,068
Mji wa DSM unazidi kukua, na usafiri wa umma(Rapid Bus Transport) bado ni ndoto.
Ongezeko kubwa la Bodaboda na Bajaja unajitahidi kuziba tatio la usafiri wa haraka hasa foleni jijini.
Lakini huu ni safiri kwanza ni wa roho mkononi kwa watumiaji, na pili kero kubwa kwa watumiaji wengine wa barabsra,maana hawafuati sheria zozote.
Mbaya zaidi wengi hawana bima wala leseni.
Polisi wa Traffic wapo, lakini nso ninkamavtstizo hilo limewazidi kimo kulingana na mspungufu yabkujipanga kwao.
SASA MAPENDEKEZO:
1. WAWEPO POLISI MAALUM WA BODA BODA NA BAJAJ
Hawa wapate mafunzo maalum kudhibiti makosa ya bodaboda na bajaj. Hapa kuna fine nyingi sana zitakazoweza kulipa mishahara yao.
2. KILA MAKUTANO MAKUBWA YAWE KITUO CHA TRAFFIC.
Makutano ya Chang'ombe-Machinjio, Kilwa rd/Mandela, Kamata/Nyerere rd, ali Hassan Mwinyi/Bibi Titi , Morocco/Bagamoyo rd, Mwenge/Bagamoyo rd Ububgo/Mandela, Magomeni/ Morogoro rd
Haya ninmakutano makuu yanaweza kutumika kudhibiti kero za bajaj/ bodaboda.
Polisi waweke kituo mobile kila makutano makubwa kudhibiti bodaboda na bajaj. Kila kituo kiwe na askari hata 15-20, ili upate askari 5, kila njia(njia ziko 4).
Kila njia idhibitiwe, helmet zivaliwe, mishkaki idhibitiwe, kuheshimu taa za kuongoza vyombo vya moto isimamiwe. Bima na leseni ziksguliwe vile vile.
Tuanzie hapo.
Polisi Traffic lazima wawe wabunifu na wasikariri mazoea.
Nchi ndogo kama Rwanda wameweza, sisi tunashindwa nini?