Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Tumesikia hivi karibuni, tangazo la Polisi Trafiki kupitia kwa Kamanda wa Trafiki Ramadhani Ng'azi kuwa dereva aje na leseni, kitambulisho cha NIDA, kitambulishi cha mlipa kodi TIN, cheti cha afya na shada ya shule aliyisomea udereva!
Kwa hayo masharti tu, unagundua kuwa kitengo chetu kina tatizo kubwa. Kwanza hawakujitayarisha kiutendaji kwa zoezi. Unachohitaji hapo ni namba ya leseni tu iliyosajiliwa na TRA. Ukiacha cheti cha afya, vingine vyote unavipata kwa mtandao.
Zoezi hili linaweza kuwa mtambo wa rushwa kwa Askari wa Trafiki.
Kamanda IGP alitazame hilo kwa makini.