Polisi, Tume ya Uchaguzi, na Kamati za Ulinzi na Usalama Dar vinara wa kufanya uovu wa kimfumo: Tunakwenda wapi baada ya hapa?

Doctor Mama Amon

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
3,513

RC Chalamila akipiga marufuku mikutano ya kisiasa eneo la Kariakoo pasipokuwa na mamlaka ya kisheria kufanya hivyo ​

Uovu binafsi hutendwa na mtu mmoja mmoja kutokana na maamuzi ya mtu mmoja huyo.

Lakini, uovu wa kimfumo hutendwa na watumishi wa taasisi kutokana na maamuzi ya vikao vya ndani ya taasisi husika.

Mifano ya uovu ya kimfumo nchini Tanzania hii hapa:
  1. Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linaamua kumwua Mwandishi wa Habari, Daud Mwangosi, kwa kutumia bomu la machozi, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  2. Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma wanaamua kufanya kitendo cha “mwangosification” dhidi ya Lissu, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, lakini walinzi wa Lissu kwa umahiri mkubwa wanafanikisha “neutralization” kwa kutumia mbinu za kikomandoo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika..
  3. Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Dar, chini ya Chalamila, wanaamua kumzuia Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya mkutano Kariakoo, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  4. Jeshi la Polisi Dar wanaamua kuzunguka na Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwa masaa Matano, kisha wanamtelekeza, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  5. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaamua kuizuia Chadema kushiriki uchaguzi, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  6. Wakurugenzi wa Halmashauri wanaamua kukata majina ya wagombea wa upinzani, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
Matendo yote haya yanayotokea ni makosa kikatiba na kisheria, lakini hakuna mtu anayethubutu kuchukuliwa hatua.

Takukuru wanayo mamlaka ya kuchunguza matukio haya na kuchukua hatua stahiki, lakini hawawezi.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora wanayo mamlaka ya kuchunguza matukio haya na kuchukua hatua stahiki, lakini hawawezi.

Rais aliyekula kiapo cha kulinda, kuhifadhi na kutunza Katiba ya nchi yuko kimya.

Leo nimemsikia Rais Samia, wakati wa uzinduzi wa toleo la 2023 la sheria zote 446, akisema kwamba: "sheria ni kioo cha ustaarabu wa Taifa."

Majuzi nimeona mtandaoni Rais Samia akinukuliwa kusema kwamba, "haki ikivunjwa amani hutoweka."

Lakini je, anaongelea haki gani hizo, kama sio haki zote zilizo kwenye katiba aliyoahidi kuitetea?

Mbona kioo anachokiongelea hawakitumii kina Chalamila ili waweze kuona makovu yaliyoko kwenye mapaji ya nyuso zao na kujisahihisha?

Je, wahusika wa uovu wa kimfumo ni kikundi cha watu walioamua kujiweka juu ya sheria kwa ajili ya kutafuta maslahi binafsi, kwa sababu hawagusiki wala kukamatika?

Kama hivyo ndivyo, tunakwenda wapi baada ya hapa?

John Heche, Makamu Mwenyekiti Chadema, akieleza ukatili waliofanyiwa na Jeshi la Polisi jana
​
Wataalam wa teolojia ya ukombozi hujenga hoja kwamba dhambi sio kitendo cha mtu mmoja mara zote kwani pia kuna dhambi zinatendwa na makundi ya watu.

Wanaelekeza nguvu zao katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii inayokumbatia dhambi za kimfumo, kama vile ukosefu wa usawa, ukandamizaji, na dhuluma, wakitaka mifumo hiyo ibomolewe na kujengwa upya. Mfano mzuri ni Prof Gustavo Gutierez (pichani) wa Amerika ya Kusini.

1745432487315.png

Prof Gustavo Gutierez, mwandishi wa kitabu, A Theology of Liberation ()--Attached

Mfano mwingine mzuri wa wanateolojia wa ukombozi ni Prof Leonard Boff (pichani) wa Amerika ya Kusini pia.​

1745432633948.png

Prof Leonard Boff​

Mawazo ya wanateolojia hawa hayana tofauti sana na fikra za wataalam wa falsafa ya ukombozi wanaoongelea uovu wa kimfumo badala ya kutumia maneno dhambi ya kimfumo. Mfano mzuri ni Profesa Enrique Dussel (pichani) wa huko Amerika ya Kusini.

1745432328576.png

Prof Enrique Dussel, ni mwandishi wa kitabu, Philosophy of liberation (New York: Maryknoll, 1985)--Attached​

Wako wapi wataalam wa teolojia ya ukombozi wa Tanzania?

Wako wapi wataalam wa falsafa ya ukombozi wa Tanzania?
 
Attachments

View attachment 3313219

Uovu binafsi hutendwa na mtu mmoja mmoja kutokana na maamuzi ya mtu mmoja.

Lakini, uovu wa kimfumo hutendwa na watumishi wa taasisi kutokana na maamuzi ya vikao vya ndani ya taasisi husika.

Mifano ya uovu ya kimfumo nchini Tanzania hii hapa:
  1. Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linaamua kumwua Mwandishi wa Habari, Daud Mwangosi, kwa kutumia bomu la machozi, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo.
  2. Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma wanaamua kufanya kitendo cha “mwangosification” dhidi ya Lissu, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, lakini walinzi wa Lissu kwa umahiri mkubwa wanafanikisha “neutralization” kwa kutumia mbinu za kikomandoo.
  3. Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Dar, chini ya Chalamila, wanaamua kumzuia Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya mkutano Kariakoo, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo.
  4. Jeshi la Polisi Dar wanaamua kuzunguka na Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwa masaa Matano, kisha wanamtelekeza, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo.
  5. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaamua kuizuia Chadema kufanya uchaguzi, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo.
  6. Wakurugenzi wa Halmashauri wanaamua kukata majina ya wagombea wa upinzani, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo.
Matendo yote haya yanayotokea ni makosa kikatiba na kisheria, lakini hakuna mtu anayethubutu kuchukuliwa hatua.

Sababu ni wazi: Wahusika ni kikundi cha watu walioamua kujiweka juu ya sheria kwa ajili ya kutafuta maslahi binafsi, kwa sababu hawakamatiki.

Takukuru wanayo mamlaka ya kuchunguza matukio haya na kuchukua hatua stahiki, lakini hawawezi.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora wanayo mamlaka ya kuchunguza matukio haya na kuchukua hatua stahiki, lakini hawawezi.

Rais aliyekula kiapo cha kulinda, kuhifadhi na kutunza Katiba ya nchi yuko kimya.

Tunakwenda wapi baada ya hapa?
Sawa
 
View attachment 3313219
RC Chalamila akipiga marufuku mikutano ya kisiasa eneo la Kariakoo pasipokuwa na mamlaka ya kisheria kufanya hivyo ​

Uovu binafsi hutendwa na mtu mmoja mmoja kutokana na maamuzi ya mtu mmoja huyo.

Lakini, uovu wa kimfumo hutendwa na watumishi wa taasisi kutokana na maamuzi ya vikao vya ndani ya taasisi husika.

Mifano ya uovu ya kimfumo nchini Tanzania hii hapa:
  1. Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linaamua kumwua Mwandishi wa Habari, Daud Mwangosi, kwa kutumia bomu la machozi, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  2. Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma wanaamua kufanya kitendo cha “mwangosification” dhidi ya Lissu, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, lakini walinzi wa Lissu kwa umahiri mkubwa wanafanikisha “neutralization” kwa kutumia mbinu za kikomandoo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika..
  3. Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Dar, chini ya Chalamila, wanaamua kumzuia Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya mkutano Kariakoo, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  4. Jeshi la Polisi Dar wanaamua kuzunguka na Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwa masaa Matano, kisha wanamtelekeza, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  5. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaamua kuizuia Chadema kushiriki uchaguzi, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
  6. Wakurugenzi wa Halmashauri wanaamua kukata majina ya wagombea wa upinzani, pasipo mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo, na hakuna hatua yoyote dhidi ya wahusika.
Matendo yote haya yanayotokea ni makosa kikatiba na kisheria, lakini hakuna mtu anayethubutu kuchukuliwa hatua.

Takukuru wanayo mamlaka ya kuchunguza matukio haya na kuchukua hatua stahiki, lakini hawawezi.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora wanayo mamlaka ya kuchunguza matukio haya na kuchukua hatua stahiki, lakini hawawezi.

Rais aliyekula kiapo cha kulinda, kuhifadhi na kutunza Katiba ya nchi yuko kimya.

Je, wahusika ni kikundi cha watu walioamua kujiweka juu ya sheria kwa ajili ya kutafuta maslahi binafsi, kwa sababu hawagusiki wala kukamatika?

Kama hivyo ndivyo, tunakwenda wapi baada ya hapa?

View attachment 3313236
John Heche, Makamu Mwenyekiti Chadema, akieleza ukatili waliofanyiwa na Jeshi la Polisi jana​
Nchi imeoza
 
Back
Top Bottom