Polisi: Tunachunguza Vijana Jamii ya Kimasai kuvamia wenzao wa Jamii ya Kimasai eneo la Kimnyaki - Arumeru

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
​
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio lililotokea tarehe 03.11.2026 muda wa asubuhi baada ya kundi la vijana jamii ya Kimasai kudaiwa kuvamia maboma ya jamii nyingine ya Kimasai na kuchukua mifugo huko katika Kijiji cha Kimnyaki, Wilaya ya Arumeru mkoani humo.

Pia soma ~ Wamasai wavamia Kata ya Kimnyaki - Arumeru wakidai ng'ombe wao walioibiwa, Polisi wapiga mabomu ya machozi

Ufafanuzi kuhusu tukio lililotokea katika Kijiji cha Kimnyaki Wilaya ya Arumeru
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio lililotokea tarehe 03.11.2026 muda wa asubuhi baada ya kundi la vijana jamii ya Kimasai kudaiwa kuvamia maboma ya jamii nyingine ya Kimasai na kuchukua mifugo huko katika kijiji cha Kimnyaki, Wilaya ya Arumeru.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni kufuatia kuibwa kwa mifugo tarehe 29.10.2026 katika Kijiji cha Lengijave na badaye mifugo hiyo kubainika ipo katika Kijiji cha Kimnyaki ambapo kutokana na mila na desturi za jamii hiyo, hawakuripoti Polisi badala yake walikubaliana kurudisha mifugo hiyo pamoja na kulipa faini kabla ya tarehe 30.10.2026.

Aidha, baada ya kushindwa kutekeleza makubaliano yao, leo tarehe 03.11.2026 kundi hilo la vijana lilivamia baadhi ya maboma katika kijiji cha Kimnyaki na kuchukua mifugo mbalimbali ikiwemo ng'ombe, mbuzi na kondoo na kuondoka nayo.

Wakati wakiwa njiani kurudi katika maeneo yao, kundi la vijana kutoka katika kijiji cha Kimnyaki walijaribu kuwazuia watu hao kabla ya Jeshi la Polisi kufika na kufanikiwa kutawanya makundi hayo ikiwa ni pamoja na kuokoa mifugo.

Katika tukio hilo hatua za haraka zilichukuliwa ikiwemo kurejesha hali ya amani katika eneo hilo, kukutana na viongozi wa kimila wa jamii hiyo pamoja na kufungua shauri la jinai kwa ajili ya uchunguzi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa wito kwa wananchi kujiepusha kuwa sehemu ya uhalifu kwa kujichukulia sheria mkononi, badala yake wanapaswa kuwa suluhisho kwa kutoa taarifa za uhalifu kwa wakati ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Imetolewa Na:
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…