DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya kiusalama nchini na kuchukuwa hatua kwa ukiukwaji wowote ule wa sheria za nchi.
Aidha, kumekuwepo na makundi mbalimbali, watu binafsi ambao wameendelea kujitokeza na kutoa matamko yenye kuashiria uvunjifu wa amani na kujenga chuki miongoni mwa jamii jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kuwa halitasita kuchukua hatua dhidi ya mambo kama hayo yenye lugha laini na nyingine kali zenye uchochezi.
Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kwa matamko na matendo yote yenye lengo la kuchochea chuki na vurugu nchini wakati huu ambao nchi ikiwa na jukumu kubwa la kuleta maridhiano ili kulinda amani na utulivu na kuendelea kukuza uchumi wetu kwani kukitokea vurugu kila mmoja wetu atapata athari hasa kiuchumi, kijamii na kiusalama.