figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu,
Mimi huwa nasafiri Mara kwa mara. Hivyo nashuhudia vifo vingi ambavyo vinatokana na watu kutokufunga Mikanda ya kwenye kiti cha Basi(Seat belt).
Imenichukua miezi minne nikifuatilia mambo ya Barabarani, ikiwemo, Rushwa, alama za barabara potofu, Matuta, Miundombinu na Watengeneza barabara ili kujua chanzo cha ajali. Kazi imeshakamilika hivyo nitapost Thread moja baada ya nyingine kama Ushauri kwa Serikali. Leo tunaanza na Mikanda.
Wakuu kuna tatizo la Watu kutokufunga Mikanda, matokeo yake ajali ikitoka wengi wanakufa. Pia barabara zetu zina matuta mengi, mtu hajafunga mkanda anarushwa hadi kuumia, wengine wakirushwa wanakalia watoto na kuwavunja wengine wanamwagiana vinywaji nk.
Tujikite kwenye Kufunga Mkanda wa Usalama. Nimegundua watu wengi hawafungi Mkanda wa Usalama. Askari wa barabarani wanaingia kwenye basi na kusema fungeni Mikanda na kushuka ila hawajui tatizo. Tatizo la watu kutofunga Mikanda ni:
1). Watu hawajui kutumia mikanda hasa kupunguza na kuongeza Urefu wa Mkanda hata kufunga na kufungua Lock.
2). Askari wa Barabarani wanasema fungeni Mikanda ila hawahakikishi kama kweli watu wamefunga Mikanda
3). Mabasi mengi hayana Mikanda na yenye Mikanda haifungu, haina lock.
4). Askari wa barabarani wamejenga sana Urafiki na madereva, hivyo anayeingia kukagua Mikanda anaishia kupiga story na Kondakta na Dereva na kushuka. Hawafanyi kazi yao Vizuri(Uzembe)
5). Magari yanajaza abiria kuliko viti vya gari. Ni kinyume na Sheria ila Polisi Wanafumbia macho.
6) Wafanyakazi wa Vituo vya Mizani wanaruhusu watu kushuka kwenye Basi na kupanda baada ya Basi kuvuka Mizani.
7). Wamiliki wa Mabasi wamejenga Urafiki na Viongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi. Trafiki akikamata Basi anapigiwa simu na Boss wake analiachia.
8). Mabasi chakavu kuendelea kufanya kazi na Polisi kutochukua hatua. Mabasi mengine yana viti na Vigoda ndani. Kigoda atafungaje Mkanda.
Nini kifanyike? Kinachotakiwa kufanyaka ni kufanyia kazi hayo hapo Juu.
Hapa Chini naweka Mabasi Mawili. Moja halina halinda Mikanda hadi Dereva hana Mkanda lipo barabarani. Basi lingine mikanda ipo lakini haina sehemu ya kufungia.
So naweka hapa Picha kama changamoto kwa Polisi ili tuone kama itafanyiwa kazi.
Ombi kwa Polisi: Tunaomba mtuonee huruma abiria. Tuna familia na ndugu wanaotutegemea. Tunaomba Mikanda ifanyiwe kazi.
Tukutane Mada ijayo.
Nakala kwa;
Simon Sirro.
David Misime
Mrakibu wa Polisi (SP) Mosi Ndozero
(Chief Of Traffic Control and Management)(DCP)Lucas Mkondya
Na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP)Willbroad Mtafungwa
Haya ndo Mabasi ambayo moja halina Mikanda kabisa hadi Dereva hana Mkanda na lingine Mikanda mibovu haifanyi kazi, huwezi ifunga kuongeza wala kupunguza.