Polisi Uganda: Bobi Wine hakupigwa risasi, alijikwaa

Polisi Uganda: Bobi Wine hakupigwa risasi, alijikwaa

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Polisi nchini Uganda wamekanusha madai kwamba kiongozi wa upinzani, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, alipigwa risasi Jumanne jioni, badala yake, wamesema kwamba kiongozi huyo wa National Unity Platform (NUP) alijeruhiwa wakati akijaribu kuingia kwenye gari lake.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Kituuma Rusoke, amesema maafisa wa polisi waliokuwepo eneo hilo wanadai kuwa Bobi Wine alijikwaa wakati akijaribu kuingia kwenye gari lake na kupelekea jeraha hilo, ingawa Bobi Wine na timu yake wanasisitiza kuwa alipigwa risasi.

Screenshot_20240904-145856.jpg

Taarifa ya Polisi inaeleza kuwa Bobi Wine na timu yake walipanga maandamano hadi mji wa Bulindo licha ya polisi kupiga marufuku maandamano hayo, ambapo alipata majeraha wakati wa mvutano na polisi.

Source: Jambo TV Online

Mnadhani nani anasema ukweli? Serikali ya Uganda au Bobi Wine?

Soma: Bobi Wine apigwa risasi ya mguu katika vuta n'kuvute na polisi
 
Serikali ya Uganda inasema ukweli wake ila ukweli huwa unajitegemea na inawezekana ukweli wa serikali ya Uganda ukawa ndiyo uongo wa ukweli wa tukio lenyewe...
 
Back
Top Bottom