Phlagiey
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 3,487
- 1,661
Kwa wengi Hushpuppi alionekana kuwa ni mfano halisi wa mtu aliyefanikiwa,mtafutaji aliyezikamata pesa za kutosha na kutokuzionea huruma katika kuzitumia, kwenye akaunti yake ya instagram yenye followers million 2.4 na ikiwa na tiki ya sawati(blue) kumejaa picha za kuvutia za Hushpuppi, akiwa mbele ya magari ya kifahari na private jet " Na mafanikio yasiwe hadithi ya zamani za kale kwako, asante Mungu kwa baraka nyingi katika maisha yangu, endelea kuwaaibisha wale wanaongoja niaibike" Aliandika Hushpuppi ikiwa post yake ya mwisho katika ukurasa wake wa instagram aliyoiweka jun 6,2020, maneno hayo yanasindikiza picha ya gari jeupe aina ya Rolls royce moja ya magari ya kifahari kabisa duniani, hilo ni moja tu kati ya magari yake mengi ya bei ghari yakiwemo; Ferrari, bugatti, mercedes-benz na magari mengine ya bei mbaya.
Huyu siyo mtu wa kusafiri kama watu wengine, ni mwendo wa private jet na safari kwake hazikauki waweza kumuita raia ya wa angani, maisha yake ni kukata mawingu akitokea Dubai kwenye makazi yake kwelekea kwenye miji mikubwa duniani kwenye biashara zake, ambazo kwa mujibu wa akaunti yake ya Instagram ni biashara ya mali zisisohamishika kama vile aridhi na nyumba yani (real estate) si mtu wa kuvaa nguo za bei chee.
Hushpuppi hutinga viwalo vya kishua kutoka kwa chapa maarufu duniania Kama; Gucci, Fendi, Louie Vito, Balenciaga na zingine, viatu, saa,mabegi na kila kitu chake anachokitumia bei yake sihaba,na ndio maana vijana wengi waliyatamani maisha yake, ndoto zao zilikuwa kuyapata maisha anayoishi walau kwa uchache tu,make yake yalikuwa hayakamatiki, pamajo na kuwepo mashaka juu ya chanzo cha utajiri wake Hushpuppi alikuwa ni role model wa vijana wengi, lakini jun mwaka huu siri kubwa iliyokuwa imejificha nyuma ya maisha yake ya kifahari ikaanikwa hadharani.
Hushpuppi, raia wa Nigeria ambae jina lake halisi ni Raymond Egbalode ni tapeli gwiji wa mtandaoni, alijipatia mamillioni ya Dollar kwa watu wengi duniani kwa njia ya uraghai akiwa kitovu cha genge zito la wezi wa mtandaoni, Hushpuppi amejihusisha katika vitendo vya utakatishaji fedha, ulaghai wa mtandaoni na kwenye bank, wizi wa utambulisho wa watu na kazi nyingi chafu zilizompa maisha ya kifahari.
Wahenga walisema siku za mwizi ni arobaini, lakini vijana wa wasasa wanasema siku ya mwizi ni aliyokamatwa, Jun 10, polisi ya Dubai walifanikisha kuwanasa Hushpuppi pamoja na watu wengine 11 wanaojihusisha na utapeli wa mtandao baada ya kufatilia nyendo zao kimya kimya kwa muda mrefu bila wao kujua, baada ya kuwepo kwa tetesi hizo kwa muda alhamis hii polisi ya Dubai ilithibitisha kukamatwa kwa genge hilo kwa kuachia video ambayo imeonesha kila hatua ya namna alivyokamatwa, Pamoja na Hushpuppi pia amekamatwa tapeli mwingine maarufu aitwaye Orale Khan Jacob a.k.a woodbelly raia wa Nigeria.
Hushpuppi na wenzake wamekamatwa kufatia operation iliyopewa jina la fox hunt 2, ambayo imefanikisha kuunasa mtandao mkubwa wa kitapeli mtandao uliyokuwa ukifanya uharifu nje ya ujumuia ya nchi za kiarabu, polisi wamesema wamewakamata kutokana na kupata nyaraka zinazoonesha utapeli wa kimataifa uliyokuwa umepangwa vyema na uliyofanikiwa kuingiza dolla million 435 ambazo ni zaidi ya Tsh. Trillion 1 na billion 10 pesa za wahanga katika mataifa mbali mbali, Polisi ya Dubai inapingana na utakatishaji fedha na utapeli wa mtandaoni " Tunazifahamu teknolojia za kisasa na njia ambazo magenge haya huzitumia kwenye uharifu wao tunatimu ya maafisa waliyofudhu kukabiliana na uharifu wa mtandao" amesema luteni genereli wa jeshi hilo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai amesema walipokea taarifa kuhusu genge lililobobea katika wizi wa mtandaoni, genge hilo linamuhusisha Hushpuppi anaejulikana kwa kuonesha utajiri kwenye mitandao ya kijamii alikuwa anajifanya ni mfanyabiashara ili kuwaraghai wahanga duniani kote, timu ya polisi ililichunguza genge lililokuwa kilifungua akaunti katika mitandao kwa majina bandia.
Kazi iniyokuwa ikifanywa na genge hili la matapeli ni kudukua barua pepe za watu kwenye makampuni, na kutuma barua pepe feki kwa wateja wao kuwaraghai wabadili utumaji wa fedha kwenda kwenye akaunti binafsi za bank za mapateli hao badala ya akaunti halali za makampuni wanayofanya nayo biashara au kazi, walikuwa wakitengeneza na kuiga tovuti za makampuni na bank, kuiba taarifa za kadi na kuwaibia wahanga kabla ya kuzitakatisha pesa hizo..
Walipowakamata polisi waliwakuta na taarifa nyingi za watu binafsi,makampuni,bank,kadi za bank pamoja na nyaraka za utakatishaji fedha,utapeli wa mtandaoni, na kudukua akaunti za wahanga nje ya jumuiya ya nchi za falme za kiarabu, nyaraka zilizogushiwa zinahusiana na utapeli uliofanyika nje ya nchi hiyo,utapeli huo ulikuwa na thamani ya diram billion 1.6 ambazo ni zaidi ya tsh trillion moja,katika msako huo wamekamatwa na pesa tasrimu diram 150 ambazo ni zaidi ya tsh bil90.7, pamoja na kuyashikiria magari 13 ya kifahari yenye thamani ya diram mil25 ambazo ni zaidi na tsh bil15.8, Computer 21,simu 37,sd card 15, hard disk 5 zenye mafail 119580 ya kitapeli na anuani za wahanga karibu mil2
Huyu jamaa ana mengi ya kumwelezea pamoja na genge lake ila anatafutwa maeneo mengi ulaya, na marekani kwa utapeli mkubwa uliyoufanya kwa wahanga wa nchi hizo kwao Nigeria pia anasakwa kwa udi na uvumba anajulikana Kama mdukuzi anayetafutwa zaidi nchi humo, moja ya utapeli aliyofanya hivi karibuni Nigeria wa dola mil35 unaohusiana na mashine ya kusaidia wagonjwa wa covid-19 kupumua zijulikazana Kama ventilator
Hivyo huko pia ana kesi ya kujibu kwa Sheria za Dubai makosa ya mtandao kifungo huanzia mwezi mmoja,miezi 3 mpaka miaka 6 kwa makosa makubwa ya utapeli Kama huu wa akina Hushpuppi, kwa baadhi ya followers wake wa instagram watakosa zawadi za pesa alizokuwa akiwamwagia mara kwa mara,lakini kwa wengine funzo kubwa ambalo watabaki nalo kwenye chanuko na anguko la Hushpuppi ni kuwa siyo kila maisha ya kifahari ambayo baadhi ya watu mashuhuri huyaonesha kwenye mitandao ya kijamii yametokana na biashara au kazi halali, kwa wengine mfano wa Hushpuppi utajiri wao umetokana na machozi ya pesa za watu walizozisaka kwa jasho na mateso makubwa lakini zikaja kuporwa na utapeli mkubwa unaotumia akili kubwa.
Machozi ya wahanga hawa waliyopokonywa Mali zao hayatapotea bure, Japo fedha zao hazitarudi uchungu na hasira za kutapeliwa utapozwa kiasi chake na taarifa za genge hili kukamtwa na vyombo vya dora
Tuwe makini MTANDAO ni dunia nyingine ambayo watu huishi na kupanga mipango yao ya kila siku, unapongia mtandano acha akili yako ya kawaida unayotumia katika dunia unayoishi,usiamini kila unachokiona na kusikia.
Kawaida ya matapeli kitu Cha kwanza ni kukujengea imani yuko tayari kufanya chochote tu ili uamini kile anachokuambia au unachokiona na kadri unavyoona vitu vyake tofauti ndivyo unavyozidi kumwamini..
Mifano ya watu Kama akina Hushpuppi wapo wengi hata Tanzania na hata humu jf wapo wengi, uchumi katika dunia ya leo ni Kama vita katika hii vita adui Yuko tayari kutumia silaha yoyote ilimradi tu akushinde .
karibuni kwa mawazo..