Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu

Kama kuna ulakini kwenye elimu yetu, elimu yako pia ina ulakini pia na uliyoyaandika yana ulakini kwa sababu elimu yako ina ulakini.
 
Huko ndiko wananchi wanajitambua sasa sio sisi huko Tzn mijitu kama Hamza nk inavyka mipaka tunaichekea eti hatuna habari nao..

Natamani siku Hawa tunaojifanyaga ni ndugu zetu waje wakiwashe tudondoke kama buku hivi ndio akili zitakaa sawa kwamba mgeni yoyote sio wa kumchekea..Ni Tzn pekee ndiko akiingia mtu asiye Raia watu hujifanya hayawahusu.
 
Bado Haijafahamika walikopata utaratibu huo wa kuingia nchi ya watu kutafuta wahalifu huku Nchi ya Malawi ikiwa na Polisi wake , hata hivyo tunaishukuru serikali ya Malawi kwa kuwanusuru na vifo baada ya kuingilia kati kuwaokoa .[emoji23]
 
Kazi nzuri, kihere here ni tabia mbaya maishani sio siri! Asante wana Lilongwe😅
 
Hao ni mashujaa kama Shujaa Hamza. Ahsante sana Wamalawi.

 
Malawi ni taifa masikini na dogo Ila watu wake wanajielewa sana. Wamejenga taasisi imara na wanaziheshimu taasisi zao. Nadhani hata raia wanayo elimu ya uraia kwa wingi wao. Hongera Wamalawi kwa kuwakumbusha polisi wetu kuheshimu sheria bila shuruti.
 
Jf sijui inaelekea wapi? Watu badala ya kuhoji kwanza chanzo cha habari wanabaki kurukia na kushadadia wasiyoyajua tu!
 
Hao shule ndogo sidhani hata kama waliwahi pigwa msasa juu ya jambo hili!!?
 


Elimu, elimu, elimu ndugu zangu ni muhimu
 
Niliwahi kushangaa kusikia wanachofanya huko Isongole nilishangaa sana nikasema hawa kwa Wamalawi ipo siku watapoteza maisha harafu hayo maeneo watu wanaishi hivyo miaka nenda miaka rudi wao mtu akibeba karanga tuu za kutoka upande wa Malawi analetewa usumbufu kwenye sukari ndio kabisaa hata za matumizi ya nyumbani naona waliamua kuvuka mpaka kupitia porini kule ili wapate zaidi..
 
Si ajabu walienda kupekua gongo malawi wakati kule gongo ni sawa na pepsi tuuu mnaweza mkakaa na mkawa mnakunywa na polisi... Yaani gongo kule ni halali..[emoji3][emoji23][emoji1787]
 
Bahati yao labda wana ushirikiano na polisi wa upande wa pili, otherwise hilo ni suala kubwa sana kama mataifa yangekuwa mahasimu...
 
Wangeyapiga wayaue kabisa,

Hakuna kitu hapo, shuleni yalikuwa vilaza,yakafeli,kazi yamepata kimagumashi,kisa mjomba,shangazi ni polisi,yaani zile reject za shuleni ndio huperekwa polisi.

Alisema Prof Assad, asilimia 60 ya watumishi wa umma ni vilaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…