Polisi waanza msako kuwatafuta Wamasai waliomshambulia dada yao kwa kukataa kuolewa na mwanaume waliomchagulia

Polisi waanza msako kuwatafuta Wamasai waliomshambulia dada yao kwa kukataa kuolewa na mwanaume waliomchagulia

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Polisi Nchini Kenya wameanza msako wa kuwatafuta Watuhumiwa watatu Wanaume kutoka kabila la Wamasai huko Nkareta, Kaunti ya Narok Kaskazini, kwa kosa la kumshambulia kwa fimbo Dada yao kisa amekataa kuolewa na Mwanaume waliyemchagua wao.

Video ya tukio hili iliyosambaa mitandaoni imemuonesha Mwanamke huyo akishambuliwa na Wanaume hao kwa fimbo kitendo ambacho kimezua gumzo na hasira na kutafsiriwa kuwa ni unyanyasaji ambapo kwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Narok.

Vyombo vya Habari Kenya vimeripoti kuwa Mwanamke huyo aitwae Lepeita ni Mjamzito ambapo Wanaume hao walimshambulia bila kujali hali yake hiyo kile walichodai kuwa hawataki aolewe na Mwanaume wasiyemkubali na kwamba tayari walikuwa wakilazimisha kuolewa katika familia waliyokuwa wanaitaka wao.

 
Huwezi ukailazimisha punda ya jirani kuipandilie yako.
 
Back
Top Bottom