Polisi wadai posho baada ya kuua!

Polisi wadai posho baada ya kuua!

nsami

Senior Member
Joined
Jun 11, 2010
Posts
175
Reaction score
8
Wakuu salaam,

Polisi waliopelekwa Iringa mwaka jana kutoka mikoa ya jirani ikiwa ni pamoja na Dodoma,
ili kuidhibiti CHADEMA wanadai kutolipwa posho yao! Waliahidiwa kulipwa 45,000 kila mmoja kwa siku na walikaa siku 10.

Polisi wanaodai kutolipwa ni waliotoka mkoa wa Dodoma ambao walipelekwa 27 kwa shughuli hiyo maalumu.
Haijafahamika kwa haraka ni kwa nini hawajalipwa posho zao hizo pamoja na kutekeleza walioagizwa kwa ufasaha.
Ikumbukwe ni katika kazi yao hiyo ndipo ndugu Mwangosi aliuwawa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kurushwa kwa mkono akiwa mikononi mwa polisi hao!

Source: Mwananchi.

link Polisi waliosambaratisha Chadema mkoani Iringa wadai posho zao - Siasa - mwananchi.co.tz
 
Kamanda wa polisi wa wakati ule kutoka mkoani Dodoma alikana kuwa hamna askari kutoka mkoani kwake aliyepelekwa Iringa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma wa sasa Ndugu David Misime anasema hana taarifa kuhusu malipo hayo hasa ikizingatiwa kuwa yeye ni mgeni mkoani humo na hajui chochote kuhusu askari walioenda huko Iringa, sasa hapa ni nani wa kumwamini kati ya polisi waliotoa malalamiko au ni makamanda wao?
Ila ripoti ya kamati Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyoundwa na kuchunguza tukio hilo ambalo lilipelekea kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi , ilisema Mwangosi aliuawa kwa makusudi na polisi chini ya usimamizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda.
Je,kamati iliyoundwa na Jeshi la polisi inasemaje?
 
Back
Top Bottom