Polisi wafafanua tukio la Wakili Lusako Alphonce kukikimbizwa na Polisi katika Ofisi za "Reachout Tanzania"

Polisi wafafanua tukio la Wakili Lusako Alphonce kukikimbizwa na Polisi katika Ofisi za "Reachout Tanzania"

View attachment 3169735
TAARIFA KWA UMMA
Taarifa iliyo upande wa kushoto inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi lingependa kuitolea ufafanuzi ili isiendelee kuleta taharuki ambayo si ya lazima.

Ni kweli Askari Polisi walifika eneo hilo kumkamata mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mweta, ambaye awali alikamatwa na baada ya kudhaminiwa aliruka dhamana kwa muda mrefu.
Leo Desemba 5,2024, Mlalamikaji alitoa taarifa Polisi kuwa, amemuona mtuhumiwa huyo, ikabidi askari wawahi haraka kumkamata.

Tunaendelea na uchunguzi kubaini ni nini kilichomfanya anayetajwa kwa jina la Alphonce Lusako kukimbia kisha kujirekodi video voice na kuirusha kwenye mitandao wakati siyo yeye aliyekuwa anatafutwa na Askari waliofika pale walijitambulisha kwake na kumweleza wamefika pale kwa nia ya kumtafuta Emmanuel Mweta.
Imetolewa na:

David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

Pia soma ~ Makumbusho: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za "Reachout Tanzania", wakidai kumtafuta Wakili Lusako Alphonce
Huyu Lusako atakuwa anamatatizo ya akili siyo mara yake ya kwanza kuleta taharuki.
 
Nyie wote mnaoishi Tanzania ni watumwa.
We mtumwa unachoongea nakuunga mkono. Heri uwe "mtumwa" anayethaminika, mwenye haki sawa na wenye nchi kasoro kuchagua na kuchaguliwa, kuliko kuishi kama mfu kwenye unsyojidangganya ni yako huku ukiwa huna haki yoyote bila connection, hata haki ya kuchagua, kuchaguliwa na kutoa mawazo nayo hawana haafu wanajiraji wapo nyubani, nyumbani my foot
 
download (1).jpg
Huyu baba asipotubu dhambi za uongo ulio kubuhu basi siku ya kiama ajiandae kuchomwa moto wake malaika wa adhabu watatumia Chlorine Trifluoride (ClF3). Yaani muende kumkamata mhusika mwingine kisha muondoke na gari ya mtu mwingine?.
Shuhuda kahojiwa na Jambo tv anasema polisi aliyekuwa na kitambulisho alisema wazi kuwa wamekuja kumkamata mtuhumiwa anaitwa Lusako. David Misime tubu mapema kabla hayajakukuta.
 
Polisi bana 🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Yaani kwenye taarifa yao wameshindwa kutoa hata namba ya jarada la kesi ya mtuhumiwa ili tujiridhishe kuwa ni kweli alikua na kesi. 🤣🤣🤣🤣🤣
Sasa tumekuwa kama channel ya vituko vya majonzi!
 
Hapa ndipo nawahurumia polisi maana itafika mahali wakiingia hata baa kwa nia njema watu wanaweza wakatoka nduki.Kwa hofu ambayo imeshajengwa kwenye jamii.Hebu washauri wa nchi hii washauri watu kabla mambo hayajaharibika zaidi.
 
Back
Top Bottom