Polisi: Wafanyabiashara wawili waliodaiwa kupotea Songea, waliuawa na Mganga wa Kienyeji na kuzikwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Jeshi la Polisi limeleza kuwa Wafanyabiashara Raymond Hyera maarufu Ray (25) na Riziki Mohamed (30) wa Songea, Ruvuma waliokuwa wamepotea walienda kwa Mganga kupata dawa ya kuwezesha biashara zao kufanya vema zaidi ambapo walinyweshwa maji yaliyowafanya walegee na kupoteza maisha na kisha Mganga kuwazika katika pori la Mdinguli.



Soma Pia:
 
Daaah yaani Tanzania yetu hii jamani vituko haviishi. Yaani mganga awape wateja wake maji wanywe walegee hadi kufa halafu akawazike kwenye pori la hifadhi. Hizi mtu mmoja kuzika watu wawili mnaona ni jambo jepesi.
 
Waganga hao waliwapa sumu dalali wa mchongo ni huyo rafiki yao...... so walipewa sumu wafe .....
 
Daaah yaani Tanzania yetu hii jamani vituko haviishi
Yaani mganga awape wateja wake maji wanywe walegee hadi kufa halafu akawazike kwenye pori la hifadhi.
Hizi mtu mmoja kuzika watu wawili mnaona ni jambo jepesi
Nini kinachoshindikana ikiwa waganga wanawasaidizi wao.
 
Haya sasa waganga wamefikiwa, swali chokonozi? Je waganga wanapelekewa na nani hao watu wa kutoa kafara?
 
Pamoja na polisi kujisafisha lakini ukweli na wao wanaohusika Kwa baadhi ya mauaji.mfano Kuna Ile kesi ya polisi kumuua mfanyabiashara wa madini mtwara ilitokea kipindi Cha Siro akiwa mkuu wa polisi lakini Hadi Leo wamekaa kimya .Na Dpp kaamua kuifuta hiyo kesi Kwa kutumia mamlaka yake ya kuweza kufuta kesi yoyote pasipo kuhojiwa na mtu yeyote.kumbuka Dpp mara nyingi Huwa ni haohao polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…