Polisi: Wafanyabiashara wawili waliodaiwa kupotea Songea, waliuawa na Mganga wa Kienyeji na kuzikwa

Umefanya biashara kwa mbinu zako umepata milioni kumi badala ya kuboresha mbinu na kujifunza maarifa mapya unaenda kwa mganga
Mganga anawaka tamaa anakupa sumu unakufa anachukua milioni kumi zako.
Elimu elimu elimu
Mganga anakaa nyumba ya tope
 
Tatizo ni elimu duni za wafanya biashara walio wengi. Mganga mchafu masikini anakupa hilizi anakuambia ilinde isinyenshewe na mvua, ni akili hiyo hilizi itanolinda je wakati haiwezi kujilinda yenyewe.
 
Umefanya biashara kwa mbinu zako umepata milioni kumi badala ya kuboresha mbinu na kujifunza maarifa mapya unaenda kwa mganga
Mganga anawaka tamaa anakupa sumu unakufa anachukua milioni kumi zako.
Elimu elimu elimu
mijinga ndiyo iliwayo
 
Yani umeweza kupata mil. 20 kwa jitihada zako mwenyewe halafu ghafla unahisi unahitaji msaada wa mganga
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini sana suala hili la kupotea kwa watu ambalo linahusishwa na utekaji. Jeshi la Polisi kwa umahiri na weledi linazidi kutegua kitandawili cha sababu za kupotea kwa watu, tafadhali soma taarifa iliyotolewa leo 05.09.2024 na Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime,
"Jeshi la Polisi linawashikilia Mtila Ausi maarufu Shehe Mtila (Mganga wa kienyeji), Omary Abdallah na Amini Sanga kufuatia vifo vya Wafanyabiashara wawili Mkoani Ruvuma ambao ni Raymond Hyera na Riziki Mohamed waliofika kwa Mganga huyo ili kupata dawa za kuwawezesha biashara zao kufanya vizuri zaidi na wakapewa maji yaliyowafanya walegee na kufariki na kisha wakazikwa kimyakimya.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime September 04,2024 imesema “August 03, 2024 katika Kituo cha Polisi Songea Mkoa wa Ruvuma, zilipokelewa taarifa za kupotea kwa Wanyabiashara wawili toka July 31, 2024, Wafanyabiashara hao walitajwa na Ndugu waliofika kituoni kutoa taarifa kuwa ni Raymond Hyera jina maarufu Ray (25) Mkazi wa eneo la Msamala, Manispaa ya Songea na Riziki Mohamed (30) Mkazi wa eneo la Mjimwema, Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma”

“Baada ya uchunhuzi na mahojiano, Mganga na wenzake walikiri Wafanyabiashara hao kufika nyumbani kwao wakiambatana na Mfanyabiashara menzao aitwaye Amini Sanga kwa lengo la kupata dawa za kuwawezesha biashara zao kufanya vizuri zaidi, waliwanywesha maji ambayo yaliwafanya walegee na kupelekea kupoteza maisha, baada ya kufariki, waliwachukua na kwenda kuwazika katika pori la Mdinguli, kijji cha Mtangashari, Tunduru kisha kuchukua fedha walizokuwa nazo Tsh. milioni ishirini na kugawana”

“September 03, 2024, Mtila Ausi na Omary Abdallah waliwaongoza Polisi hadi walipowazika Wafanyabiashara hao, ufukuaji ulifanyika na miili ya Wafanyabiashara hao ilikutwa, uchunguzi unaendelea kukamilishwa ukiwepo wa kisayansi ili taratibu nyingine zifuate”
#MillardAyoUPDATES
 
Mgangaa njaaa huyo ..c mganga matatizoo ya watu...
 
Hii Nchi tunaishi tu kwa mapenzi ya mungu!, tuna mfumo mbovu sana wa Usalama...
Kwa hili tukio ndiyo unasema hivi? Labda mifumo mizuri ni kuwa ana askari mmoja wa jeshi la polisi kila nyumba na kufanyia ulinzi humo?

Kila nchi watu wanauana kwa bahati mbaya au makusudi, na ndiyo maana mahakama zote duniani zinazo kesi za mauaji. Ndivyo binadamu tulivyo.

Watu ambao wanaamua kivyao kukutana ndani ya nyumba kwa maelewano, wakiuana utalaumu mfumo wa usalama?

Polisi wana shida zao, lakini katika hili tulipaswa kuwapongeza japo kwa kuwapata wafanyabiashara hao, japo wakiwa wafu. Wamefanya kazi nzuri.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…