Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mwili huo unaodaiwa kuwa wa Richard Shoo, aliyefariki dunia Juni 19, 2024 ulitakiwa kufukuliwa kwa ajili ya uchunguzi na vipimo vya vinasaba (DNA), baada ya familia moja kuibuka na kudai mwili huo uliozikwa si wa marehemu Shoo bali wa kijana wao.
Baada ya sintofahamu hiyo, inadaiwa Mahakama iliamuru mwili huo ukafukuliwe, ili kufanyika kwa vipimo na taratibu nyingine za kisheria zifuate.
Hata hivyo, Polisi jana Jumapili Septemba Mosi, 2024 wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Moshi wakiambatana na madaktari wawili, walifika kwa ajili ya kufukua mwili huo, lakini ilishindikana baada ya familia kudai kutoshirikishwa na kutaka kuonyeshwa kibali cha kufukua mwili huo na polisi hawakuwa nacho.
Soma Pia:
- Kuna haja gani ya kutunza mwili wa marehemu kisa migogoro?
- Mwili wa Marehemu kufukuliwa ili uzikwe upya baada ya utambuzi
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema kazi ya kufukua mwili huo lilishindikana baada ya upande mmoja kutoridhia na baadhi ya wanafamilia kudai kutoshirikishwa suala hilo.