Polisi Wafyatua Risasi na Mabomu ya Machozi Kutuliza Waombolezaji Waliofurika kumuaga Odinga

Polisi Wafyatua Risasi na Mabomu ya Machozi Kutuliza Waombolezaji Waliofurika kumuaga Odinga

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga kwa sasa umefika katika uwanja wa michezo wa Kasarani kwa ajili ya kuagwa.

Maafisa wa jeshi wamelazimika kufyatua risasi angani ili kuwatawanya waombolezaji abao waliingia ndani ya uwanja huo kabla mwili haujafika na kuujaza uwanja wote kiasi cha kushindwa kuungiza mwili huo ndipo polisi walipotumia silaha na mabomu ya machozi kuwatawanya.

Soma Pia: Raila Amolo Odinga afariki dunia nchini India kwa mshtuko wa moyo

Rais William Ruto ni miongoni mwa waombolezaji waliofika uwanjani hapo Kasarani.

 
Wakenya ni ushamba mwingi sana,
bora watawanywe tu kinguvu.
Huo msiba badala kuenzi kwa heshima mnagalagala mnakumbatia kabati, kashakufa mzikeni vizuri,
sasa mnasindikiza mwili kwa risasi na mabomu.
 
Back
Top Bottom