Polisi waimarisha ulinzi eneo la maombi ya waumini wa Askofu Gwajima

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Leo Juni 29, 2025 eneo ambalo waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Glory of Christ Tanzania Church wamekuwa wakitumia kwa maombi, liko chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi leo Jumapili. Hali hiyo imejiri baada ya zuio la kufanya ibada katika majengo ya kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, Dar es Salaam.

Maeneo ya wazi nje ya kanisa, hasa chini ya mti na nyuma ya kituo cha mwendokasi, yameendelea kuwa sehemu ya maombi kwa waumini hao tangu zuio hilo litolewe. Hata hivyo, leo askari polisi wengi wameonekana wakilinda maeneo hayo tangu asubuhi.

Hali kama hii ilijitokeza pia Jumapili iliyopita ambapo waumini walikusanyika na kufanya ibada fupi na kutoa sadaka, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Askofu Maximilian Machumu Kadutu (Mwanamapinduzi).

Zuio hilo limekuwepo tangu Juni 2, 2025, ambapo hadi leo Juni 29, 2025, ni jumla ya siku 27 tangu zuio hilo kuanza. Waumini wamesisitiza kuendelea na maombi licha ya changamoto hizo, wakisema imani yao haitatetereka.

Jeshi la Polisi bado halijatoa taarifa rasmi kuhusu sababu ya kuimarisha ulinzi leo, huku jitihada za viongozi wa kanisa hilo kutafuta suluhu zikiendelea.
Screenshot_20250629_115955.jpg

Yeye mwenyewe Gwajima anasemaje?
 
View attachment 3388126
Polic imekosa kaz asubuhi yote Bado wanapambana nawaumini wa gwajima tu
 
Mbona imekuwa ni kisasi? Tena si na Gwaji boy, ila na waumini. Hii si sawa kabisa. Mungu anawaona.
 
Mwenyezi Mungu baba , hebu lete mvua ndogo iambatane na Radi nzito ipige na kuwasafirisha kuzimu hawa atu wanaozuia watu kuabudu.Radi ipige hapo walioweka doria na kuwasafisha wote
 
Back
Top Bottom