Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Wanawake wawili wakazi wa Mkoa wa Arusha wanashikiliwa na polisi wa Mkoa wa Manyara, kwa tuhuma za kukutwa na misokoto 1,220 ya dawa za kilevya aina ya bangi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, George Katabazi akizungumza na Mwananchi Digital leo jumanne Septemba 27 amesema wanawake hao wamekamatwa kijiji cha Mswakini wilayani Babati.
Kamanda Katabazi amewataja wanawake hao kuwa ni Beatrice Abel aliyekamatwa na misokoto 630 na Glory Samwel akiwa na misokoto 597 wote wakazi wa Ngaramtoni mkoani Arusha.
"Wanawake hao walikuwa wamepanda basi la kampuni ya KSK linalofanya safari zake kutoka mkoani Tanga kuelekea mkoani Arusha na walipofika kijiji cha mswakini ukaguzi mkali ulifanywa na polisi wakawakamata," amesema.
Kamanda Katabazi amesema wanatarajia kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao pindi uchunguzi wake utakapokamilika.
Chanzo: Mwananchi