Polisi wakimbizana na Wamachinga Dar

Ila hawa ndugu zetu wamezidi,,, services road imekuwa ndo ya kupangia biashara,,, mji unaonekana uko hovyo sababu ya hawa ndugu zetu,, yani mji haupitiki kwa miguu
 
Mbona RC ameongeza muda kwa siku 12 mbele , mashambulizi ya Polisi na wamachinga Msimbazi ni ya nini , kwanini zisisubiriwe hizo siku 12 ?
Waliwapa muda wa kuondoka kiungwana umekwisha huku biashara zikiendelea kama kawa! Sasa siki 12 za kuondolewa, si kuondoka!!
 
Machinga ni matokeo ya kushindwa kwa sera za ccm kuhusu ajira na uchumi
Hata huko unapoona nchi zilizoendelea za ulaya hao wanaofanya biashara mitaani wapo hila wanapangwa wasibughudhi wengine sio kisingizio cha ajira mpk mzibe njia za watembea kwa miguu mtu inabidi apite barabarani kupishana na magari njia ya kutembelea imejengwa mabanda
 
Kwa huu uchafu wanaojaza barabarani acha waondolewe tu.
 
ukifanikiwa kuvunja mabanda ya wamachinga yote. 75% wanafungua maduka. hao wachache waliobakia unaweza kuwapanga. weng wa wamachinga ni watu waliopata hela kilain ila wakakosa elim sahh ya hela. leo hii ni kawaida kumkuta machinga ana sim mpaka ya ml. 2.
 
Inafikia wakati mtu unajishauri kwenda kariakoo hii haiwezekani. Halafu hawa wafanyabiashara wadogo wadogo wengi hawalipi kodi.
Yaani we ndio mimi. Kila nikiwaza kwenda Kariakoo, hao jamaa wananikatishaga tamaa inaweza pita mwaka sijaenda.
 
Halafu Magufuli alikuwa anawaambia wazaliane tu.Ndo vijana wenyewe asilimia kubwa ndo machinga. Wawaondoe tu.Wataumia ila watazoea tu.Kila mtu huko mikoani anawaza kuja Dar kuwa machinga. Enough is enough. Hakuna kurudi nyuma,wawaondoe tu. Watembea kwa miguu kariakoo unatembea huku umebana pochi yako kisa mbanano. Vibanda mbele ya maduka uliona wapi ?Vibanda kwenye service road jamani 😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…