Polisi walikuwa wapi uwanja wa Taifa mpaka mashabiki wanaingia uwanjani na kung'oa nyasi bandia?

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491
Kufuatia mvua kubwa na umeme kukatika uwanja wa Taifa wakati wa mechi kati ya Simba ya Tanzania na Al Misry kutoka Misri mechi ilisimama kwa muda lakini wakati huo huo baadhi ya mashabiki waliingia eneo la kuchezea mpira yaani pitch na kuanza kucheza kwenye maji yaliyojaa uwanjani na wengine kudiriki mpaka kung'oa majani yaliyowekwa juzi tu na Serikali.

Najiuliza tu mechi kama hizo huwa tuna walinda usalama wa kutosha pale uwanjani kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayevunja amani lakini niliona mpaka vijana wanaingia uwanjani na kuanza kung'oa majani hakuna polisi aliyekuwa karibu mpaka baada ya dakika kadhaa tena uharibifu umeshafanyika ndiyo polisi wanaingia uwanjani kuwatoa na kuwakamata baadhi yao.

Vyombo vya ulinzi iwe mvua iwe jua mnatakiwa kuwa alert muda wote, kwa jana pale ni hasara kwa Taifa kwasababu lazima marekebisho yafanyike tena kwa yale maeneo ambayo majani yameng'olewa.

Na wewe mtanzania unayeingia uwanjani kwa lengo la kung'oa majani hasa maana yake ni nini? Kwanini usilinde uwanja wako tena wa kimataifa.

Tuwe na tabia ya kulinda mali za nchi
 
Mkuu hivi ushafika ata kwenye huo uwanja wa taifa? Tuanzie hapo kwanza maana kama ushafika basi utakuwa unafahamu ukubwa wake, haya jiulize ni askari wangapi ambao wanaweza kuzunguka uwanja ili watu wasipite na istoshe tatizo kubwa ni umeme ulipokatika na mvua kunyesha
 
Chadema hawakuwapo.
 
Haijalishi ukubwa wa uwanja issue ni usalama muda wote wakati wa mchi inapoendelea au lolote linapotokea na hiyo ndiyo kazi ya wana usalama wakiwa kazini.Hakuna excuse katika suala la usalama.
 
Nani kakwambia polisi shida yao kushughulika na watu kama hao,waharibu nyasi za uwanja,looooooohhh!!!!!! Kazi yao kupambana na wapinzani hasa CHADEMA.hapo utaona nguvu kubwa.
 
HAHAAA LEO WASHANGAA TAASISI ZENU JINSI ZINAVYOFNYA KAZI "" MBONA HUJUSHANGAA AKWILINA ALIVYOUWAWA NAMPAKA LEO HII WALIOMUUWA HAWAJA WAJIBISHWA WANAKULA BATA TU ""

KAMA UMESHAANZA KUHOJI KUHUSU UTENDAJI WA HIZO MAMLAKA ZENU ...NA HAKIKA UTAKUWA UMESHAANZA KUPONA KIDOGO KIDOGO ""
 
Eti tuwe na uchungu na mali za nchi, wangelijua hilo wangeacha kuzitumia hela hizo kututeka na kununua upinzani
 
Mtawaonea polisi bure!!!! simba wameshashindikana......mara warushe uwanjani chupa za maji walizojaza mikojo.......mara rambo zenye mbolea sijui ni ya nini......mara wangoe viti sasa hao ni jadi yao
mbolea ili nyasi zikue au unataka zikauke
 
Uwanja wa Taifa hauna nyasi bandia, bandia ziko uhuru.
Uwanja wa Taifa utumike mchana kwani hauna uhakika wa kupata umeme muda wote.
Umeme unapokatika uwanjani usiku ni hatari kwa washabiki na wageni kiusalama kwani watu wenye tabia mbalimbali huwepo uwanjani na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Tafadhaki tafadhali, kutokana na uwezo wa nchi yetu katika upatikanaji wa umeme naomba MECHI ZICHEZWE MCHANA.
 
Back
Top Bottom