Naombeni msaada wa kisheria juu ya hili.
Ndugu yangu kafungiwa account yake ya bank kwa amri ya polisi. isa ni kutuhumiwa aliibia kampuni hela.
Je kisheria polisi wana mamlaka hayo ya kumfungia mtu bank account na kushikilia mali zake kisa tu katuhumiwa kuibia kampuni hela??
braza ni bank gani hiyo?!?! polisi hawawezi funga akaunt ya mteja, ni amri ya mahakama ndio inaweza zuia mteja kutransact account yake.
Ni CRDB ndugu. Hatua zipi tunaweza chukua kufungua account na kurejesha mali polisi wanazoshikilia??
naomba nijue jina la hiyo bank. akaunt inafungwa 1) kwa ridhaa ya mteja mwenyewe. 2) kwa ridhaa ya bank e.g mteja anajihusisha na money laundering, 3) kwa amri ya mahakama kwa ajili ya public interest.