TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,999
- 24,328
POLISI WAMFUNGA PINGU MWANANCHI NA KUMUACHA AENDENAZO NYUMBANI.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Giles George Mkazi wa Wilaya ya Nkasi amelalamika kufungwa pingu na askari wawili wa Jeshi la Polisi (Majina Kapuni) kwa siku tatu, kuanzia Jumamosi Septemba 19 hadi Jumatatu Septemba 21, na askari hao kutokomea kusikojulikana kwa kosa ambalo halitambui.
Inaelezwa kuwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya kuhudumia Mifugo kwa Bosi wake ambaye ni Bwana Afya (Jina limehifadhiwa) tangu Julai mwaka huu, lakini hivi karibuni akawa hamuelewi Bosi wake kwani alikuwa akichukua watu wengine kufanya majukumu yake.
Anasema alipohisi ndipo Bosi wake akamwambia akiwa amechoka kufanya kazi aondoke. Kijana huyo alipodai maslahi yake akaitiwa Polisi ambao walimfunga pingu na baada ya kugundua hana hatia yoyote walimuacha na pingu zikiwa hawana funguo za kumfungua.