Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Polisi Dar es Salaam leo wamemkamata mwandishi wa habari Moshi Lusonzo, ambaye alikuwa akipiga picha wakati wa operesheni ya polisi ya kukamata wafanyabiashara wanaoiba haki za wasanii katika maeneo ya Kariakoo. Polisi hao wamemnyang'anya mpiga picha huyo kamera yake na kitambulisho wakidai kwamba wameingiliwa katika kazi zao za upelelezi.
Kabla ya operesheni hiyo, polisi hao walipiga simu jana na kutaka waandishi washuhudie jinsi polisi wanavyotekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete katika kukabiliana na wafanyabiashara wanaoiba kazi za wasanii.
Hadi sasa mwandishi huyo yuko kituo cha polisi cha Msimbazi.